Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuwashukuru wajumbe mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu kilichofanyika leo Disemba 12,2025 wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

Na.Alex Sonna-KISARAWE

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, ameanza utekelezaji wa ahadi alizozitoa wakati wa uchaguzi mkuu 2025 kupitia Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku akitaja barabara, maji, afya na elimu kuwa miongoni mwa vipaumbele vyake vikuu katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe, Dkt. Jafo amesema tayari amewasiliana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuhusu barabara ya Kisarawe, hatua inayolenga kuhakikisha mkandarasi anaanza utekelezaji wa mradi huo kwa wakati.

Katika sekta ya maji, amesema amefanya kikao na ujumbe kutoka Korea kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji utakaohusisha ujenzi wa vituo 105 vya kuchotea maji katika vijiji 17. Ameongeza kuwa ameomba kuzingatiwa kwa uwekaji wa matenki makubwa na kuangalia uwezekano wa kuvifikia vijiji vya Gwata na Dololo.

“Eneo hili linahitaji matenki makubwa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu kufuatia uwepo wa Bandari ya Kwara. Mradi huu ni mkubwa, una thamani ya takribani sh. bilioni 27, si jambo dogo,” amesema Dkt. Jafo.

Kwa upande wa elimu, amesema ataendelea kutafuta pesa Serikali kuu pamoja na wadau wengine wa elimu ili kuboresha miundombinu pamoja na ujenzi wa shule za sekondari pamoja na kuipandisha hadhi Shule ya Sekondari Jafo kuwa na kidato cha tano na sita na kuitenga kwa wavulana.

“Pia nimeomba kuongezwa kwa bweni Shule ya Sekondari Kisarawe, ujenzi wa sekondari mpya Mafizi, Maluwi, Kwala, Sungwi, Mwanzo Mgumu, Kiluvya B, Sanze na Bwama,” amesema.

Ameongeza kuwa amewasilisha pia maombi ya ujenzi wa shule mpya katika maeneo ya Kibesa, Mjimpya, Darfur na Vihingo, pamoja na kuongeza madarasa katika shule za Malumbo, Mfulu na Kibwemwenda.

Dkt. Jafo amesema pia anaendelea kuifuatilia TARURA ili kuhakikisha barabara zinakuwa katika hali nzuri, na baadhi ya barabara korofi kujengwa kwa zege ili ziweze kupitika wakati wote wa mvua.

“Naiomba CCM tushirikiane ili katika miaka hii mitano tuweze kutimiza matarajio ya wananchi. Nitaanza ziara za kushukuru awamu kwa awamu na kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu,” amesema.

Awali, amempongeza Aidan Kitare kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na kuahidi kuwa Ofisi ya Mbunge itatoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu ya chama

Pia amewashukuru wana-CCM kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuendelea kuongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano, akieleza kuwa wilaya hiyo imeendelea kuwa tulivu kisiasa.

Aidha, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kutolewa kwa fedha za serikali zilizochochea maendeleo ya Wilaya ya Kisarawe.

“Tumsaidie Rais wetu kwa kutimiza wajibu wetu. Kwa upande wangu, nitaongoza kuhakikisha malengo ya Rais kwa Kisarawe yanatimia,” amesema.

Kwa upande wake Mwewnyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kisarawe ndg.Khalfan Sika,amempongeza Mhe.Jafo kwa kazi kubwa aliyoifanya katika Jimbo la Kisarawe kwa kuleta maendeleo hivyo watampa ushirikiano wa kutosha ili aendelee kumsaidia Mhe.Rais Samia kutekeleza miradi ya wanakisarawe.


Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuwashukuru wajumbe mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu kilichofanyika leo Disemba 12,2025 wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuwashukuru wajumbe mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu kilichofanyika leo Disemba 12,2025 wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.


Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuwashukuru wajumbe mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi Mkuu kilichofanyika leo Disemba 12,2025 wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.





Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akimsikiliza Mwewnyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kisarawe ndg.Khalfan Sika,wakati wa kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuwashukuru wajumbe hao kilichofanyika leo Disemba 12,2025 wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.



Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akimsikiliza Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kisarawe Bi.Josephine Mwanga ,wakati wa kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe kwa ajili ya kuwashukuru wajumbe hao kilichofanyika leo Disemba 12,2025 wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.



Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akimsikiliza Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kisarawe, Aidan Kitare,katika kikao cha Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Kisarawe wakati wa ziara ya kutoa shukrani kwa wajumbe hao kilichofanyika leo Disemba 12,2025 wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...