-ASISITIZA KAMPASI HIYO IWE KITOVU CHA UVUMBUZI NA UBUNIFU
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametoa wito kwa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kuhakikisha Kampasi mpya ya Mkoa wa Kagera inakuwa kitovu cha uvumbuzi na ubunifu, mahali ambapo vijana watawezeshwa kuibua mawazo mapya, kufanya ubunifu, na kutumia fursa za soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mkoa wa Kagera, inayojengwa katika Kijiji cha Itawa Wilayani Bukoba. Amesema, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kihakikishe kuwa mitaala itakayotumika katika kampasi hiyo inalenga moja kwa moja katika kuleta maendeleo ya jamii kwa kutoa zaidi elimu-ujuzi, yaani mafunzo ya amali, kwa kuwa Mkoa wa Kagera na kanda yote ya ziwa ina fursa nyingi za kiuchumi.
Aidha, Makamu wa Rais amesema, kwa kuwa Mkoa wa Kagera unapakana na nchi jirani kadhaa, uwepo wa Kampasi hiyo utatoa fursa na kuvutia vijana katika nchi hizo kuja kujipatia maarifa muhimu. Amesisitiza Kampasi hiyo iwe ni mahali pa kukuza mtangamano wa Afrika Mashariki na kuendeleza umajumui wa Afrika ambao umekuwa msukumo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Vilevile, amesema ni tumaini kuwa, kupitia kampasi hiyo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitatoa mchango mkubwa katika kuendeleza maarifa katika ujasiriamali, kukuza ujuzi wa masoko, kuchochea biashara za mpakani, na kujenga uwezo wa vijana kuhimili ushindani katika soko la kikanda na kimataifa.
Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejizatiti kuendeleza jitihada za kuleta mabadiliko katika ngazi zote za elimu, hususan elimu ya juu kwa kuhakikisha kuwa wahitimu wanapata ujuzi, stadi na maarifa yanayoendana na soko la ajira.
Amesema, lengo kuu la Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (2025-2030) ni kukuza uchumi na kuimarisha ustawi wa wananchi, ambapo mojawapo ya njia ya kufikia azma hiyo ni kuongeza fursa ya elimu kwa vijana katika ngazi zote, ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu bila ada kuanzia elimu ya msingi hadi sekondari.
Ameongeza kwamba, katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na hatua nyingine imefanya uamuzi wa kuhakikisha kila mkoa hapa nchini unakuwa na ama Chuo Kikuu au tawi la Chuo Kikuu.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ambaye ni Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amesisitiza umuhimu wa kuongezwa ardhi ya kutosha katika eneo hilo la ujenzi kwani lengo la kutoa ardhi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika miaka ijayo, ni kuiwezesha kampasi ili iweze kuwa Chuo Kikuu kinachojitegemea.
Amesema Kampasi hiyo inatarajiwa kuwa na miundombinu ya kisasa na kuzingatia viwango vya kimataifa. Pia amesema kipaumbele kinawekwa kuwa na mazingira rafiki yatakayoweza kukidhi mahitaji ya watu wote hususani wenye mahitaji maalum.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...