Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Angellah Kairuki amesema kuwa baada ya kuanza kutumika kwa mifumo ya Tehama ikiwemo katika Mahakama na Mabaraza mbalimbali ikiwemo ya Ardhi kumeshuhudiwa kwa mashauri mengi kuendeshwa kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu.
Lakini pia kumeshuhudiwa kupungua kwa rushwa na kuondoka kwa urasimu katika taratibu za utoaji wa huduma na haki sambamba na kuwepo kwa mageuzi makubwa ya kukubalika kwa ushahidi wa kielektroniki.
Waziri Kairuki ameyasema hayo leo Jijini Dodoma Desemba 15,2025 akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya Vifaa vya Tehama kwa Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake.
"Kupitia Wizara yetu ya Mawasiloano na Teknolojia ya Habari tumenedelea kusimamia na kuhakikisha mapinduzi makubwa yanaenfelea kutokea kupitia Taasisi zetu za Kiserikali zikiweko Taasisi za utoaji wa haki".
"Baada ya kuanza kutumia Tehama ikiweoma katika Mahakama pamoja na Mabaraza mbalimbali yakiwemo ya ardhi tumeona mashauri mengi yakiendeshwa kwa ufanisi,ubora wa hali ya juu,kuwepo kwa uharaka,kuondoka kwa Urasimu katika utoaji wa huduma za haki,tumeona ambavyo mifumo hii imepunguza rushwa na kuelekea kuondoka kabisa,kutokuwa na msongamank wa mashauri na kuwepo kwa mageuzi makubwa ya kukubalika kwa ushahidi wa kielektroniki".
Aidha Waziri ameleeza kuwa kupitia mageuzi haya ya kidijitali lengo la Serikali ni kuona wanaendelea kujenga Serikali ya kisasa inayofanya kazi kwa ufanisi zaidi kupitia mazingira ya kidijitali na kutumia dijitali hiyo kwaajili ya kuhakikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiloano na Teknolojia ya Habari Mohammed Abdulla amesema kuwa Wizara itaendelea kuwa kichocheo cha maendeleo kama ilivyoanishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 kwa lengo la kuifikisha nchi kuwa kwenye uchumi wa kidijitali ambao unatamaniwa na wote kufika huko.
Pia Katibu Mkuu Wizara ya Katina Sheria Eliakim Maswi akiongea kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo ameeleza kuwa hatua hii ya kupewa vifaa vya Tehama inaakisi dhamira ya Serikali ya awamu ya sita ya kuimarisha matumizi ya Tehama katika utoaji wa huduma za Umma,kuongeza ufanisi lakini pia kuimarisha uwajibikaji katika Sekta ya haki na Utawala wa Sheria nchini.
Na kuongeza kuwa kupata kwa vifaa hivyo imekuwa ni chachu muhimu sana ya kuharakisha mageuzi ya kidijitali ndani ya Wizara na Taasisi zake na pia vifaa vitawawezesha kuhamia kwa kasi zaidi kutoka mfumo wa kawaida wa karatasi kwenda mfumo wa kielektroniki kama Serikali inavyoelekeza.
Akitoa salamu za Ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Serikali Bi Rehema Katuga ameshukuru kwa kupewa vifaa hivyo na kusema kuwa kwao ni chachu kubwa katika kuimarisha Ofisi yao kwani ni mpya angawa katika majukumu ni ya muda mrefu.
Naye Faith Minani ambaye ni mwakilishi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema kuwa kupata kwa vifaa hivyo vitawezesha kufanya majukumu yao kwa wepesi zaidi, huku wakijua kuwa wana jukumu kubwa la kuishauri Serikali juu masuala yanayohusu Sheria lakini pia kuwasaidia wananchi kuzijua Sheria na Stahiki zao mbalimbali.
Mkurugenzi wa Mashtaka Sylvester Mwakitalu akitoa salamu za Ofisi ya Taifa Mashtaka amesema kuwa vifaa hivi vitaimarisha juhudi ya Serikali ya kuimarisha matumizi ya Tehama katika utoaji wa haki kama ambavyo wanafanya sasa kusikiliza mashauri kwa njia ya mtandao na kusajili nyaraka mbalimbali kwenye mfumo unaoratibu mashauri.
Vifaa vilivyotelewa leo ni pamoja kompyuta mpakato 70 kwenda kwa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Taasisi zake ikiwemo Ofisi ya Mwandisi Mkuu wa Sheria,Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...