Na Said Mwishehe,Michuzi TV.
MWENYEKITI was Kituo cha wanahabari watetezi na taarifa (MECIRA) Habib Mchange amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kuacha mara moja kushawishi umma ili kuvuruga amani na utulivyo wa nchi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Mchange ametoa onyo hilo leo Desemba 12,2025 jijini Dar es Salaam na Waandishi wa habari alipokuwa akimjibu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA John Heche ambaye jana amezungumza masuala mbalimbali yanayoendelea nchini.
Miongoni mwa mambo aliyozungumza Heche no kwamba anataka kuwepo na Serikali ya mpito na kwa mtazamo wake anataka mashirika kutoka nje wapewe nchini,ambapo Mchange amesisitiza nchi ya Tanzania ni huru na Watanzania hawako tayari kuona Wazungu ndio wapewe nchi waongoze.
Mchange amesema CHADEMA imekuwa mstari wa mbele kushawishi umma na kujitafutia uhalali wa kuhamasisha vurugu na kutoa lawama zisizo na uhalali kuhusu uchaguzi mkuu uliopita mwezi Oktoba 29.
"CHADEMA walisema hawezi kushiriki uchaguzi hadi wapate mabadiliko wanayoyataka, kwa sababu wao hawajashiriki uchaguzi lakini vyama vingine vimeshiriki, watanzania wameshiriki halafu Heche anasema uchaguzi sio halali.
“Eti unasema kiongozi aliyepatikana sio halali kwasabu haujashiriki.Uhalali huo wa kulalamikia uchaguzi ambao hawakushiriki wanautoa wapi.Ninamfano Heche sifa yake moja aliwahi kuwa Mwenyekiti wa vijana CHADEMA na sisi tuliokuwa vijana wa Chama hicho wakati ule tulimheshimu.”
Aidha amesema sasa nchi inautaratibu ambao unaeleza ili ushiriki uchaguzi lazima ukasaini fomu ya maadili, sasa wao CHADEMA walisema uchaguzi hawataki na fomu hawasaini halafu wanakuja baadaye wanasema uchaguzi sio huru, uchaguzi haukuwa wa haki umeingiliwa.
Mchange amesema zipo kazi nyingi za kufanya sio lazima watumie nguvu kubwa kulazimisha kushawishi jamii iingie kwenye machafuko na kwenye hilo ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama wafanye uchunguzi wa makini waangalie namna ambavyo Chama hicho kinaweza kuwa kimehamasisha kufanikisha vurugu za Oktoba 29.
"Vyombo vya ulizi na usalama vimewachekea sana CHADEMA, hivyo niwaombe wafanye uchunguzi wa kuangalia kwa namna gani wanahusika moja kwa moja katika vurugu za Oktoba 29.
“Kwa sababu mahusiano yao na baadhi ya taasisi za ndani na nje zinafanana kwenye lugha kwamfano wanasema wapeni wananchi wazike miili yao. Ni nani ameomba mwili wake akanyimwa.Heche anasema kuna watu wamezikwa kaburi moja.
“Taarifa hiyo hiyo anaisema Heche , taarifa hiyo hiyo inasemwa na mwandishi kutoka nje, taarifa hiyo hiyo inasemwa na mwanaharakati mmoja anayeiendesha Chadema kutokea Nairobi, Kenya, taarifa hiyo hiyo inasemwa kwenye vikundi vyao, halafu na sisi huku tunamwamini.
“MECIRA tunasema hatuko tayari kuruhusu uhuru wa taifa letu, amani ya taifa letu iliyojengwa kwa zaidi ya miaka 60 ichezewe tena kama ilivyochezewa tarehe 29 Oktoba.
“Lakini tunawahoji viongozi wa upinzani hasa CHADEMA wajiangalie kama wanavyofikiri ni sawasawa? Inawezaje kuwa sawa taifa lako liongozwe na watu wa nje.”
Pia Mchange amesema jambo jingine muhimu watu kujua CHADEMA hawajaanza leo kutoshiriki uchaguzi mkuu kwani mwaka 1995 hawakushiriki uchaguzi, alikuwa mgombea Mrema na wengine kutoka upinzani uchaguzi ulikuwa huru haukuwa huru?
“Mwaka 2000 CHADEMA hawakushiriki uchaguzi mkuu, waligombea CUF, NCCR na wengine uchaguzi ulikuwa huru haukuwa huru? Kwahiyo uchaguzi kuwa huru na halali hauwezi kuhalalishwa na ushiriki wa CHADEMA.
“Wee hukushiriki uchaguzi halafu unasema serikali huitambui lakini walioshiriki wanaitambua, vimeshiriki vyama zaidi ya 15 na mbele ya sheria vyama vyote vina haki na hadhi sawa, na kwa nchi yetu suala la uchaguzi ni hiari vyama vya siasa havilazimishwi kushiriki uchaguzi. Unaamua mwenyewe ushiriki au usishiriki,”amesema Mchange.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...