Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwa hotuba yake iliyojaa hekima na weledi aliyoitoa mbele ya wazee wa Dar es Salaam.

Msama ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam,na kubainisha kuwa hotuba aliyoitoa Rais Dkt.Samia imeonesha uwazi, ufasaha na dhamira ya dhati ya kulinda amani na utulivu wa Taifa.

“Hakuna kiongozi anayetamani wananchi wake wapate shida au mashaka. Kila kiongozi mwenye busara hutaka kuona watu wake wakiishi kwa upendo, umoja na amani,” amesema Msama. Akitolea mfano kitabu cha Wafalme katika maandiko matakatifu, Msama alisema ni muhimu kwa wananchi kuheshimu maagizo na mamlaka zilizopo kwa manufaa ya Taifa.

Amesisitiza pia umuhimu wa vijana kuondoa hofu na kuendelea kuheshimu mihimili ya nchi ikiwemo Rais, Bunge na Mahakama.

Aidha, Msama aliwataka wazee kuzungumza na watoto na wajukuu wao ili kuhakikisha hawaingii katika vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani ya nchi.

“Methali inasema: ‘Asiyefunzwa na wazazi hufunzwa na ulimwengu’. Nawaomba wananchi tarehe 9 watulie nyumbani na kuendelea na shughuli zao kama kawaida,” amesema msama.

Vile vile, aliwataka viongozi wa dini kuepuka kufanya siasa madhabahuni na badala yake wahubiri injili kama alivyofanya Nabii Yona, akiwataka kutokutumiwa vibaya katika kuvuruga amani ya nchi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...