Na Mwandishi Wetu  

Serikali imesema kuwa itahakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira wezeshi ya biashara, kupata faida, na kuchangia katika ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Patrobas Katambi  alipomuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani, yaliyofanyika  Jijini Dar es Salaam.

Kauli mbiu ya mwaka huu, “Akili Mnemba (AI), Walaji na Sera za Ushindani ”, inalingana na dhana ya kimataifa ya "Artificial Intelligence (AI), Consumers and Competition Policy", ikisisitiza kuwa teknolojia ya AI ni zana muhimu katika kudumisha ushindani wa haki, kulinda maslahi ya walaji, na kuongeza uwazi katika soko.

“Serikali imejipanga kuwa daraja, si ukuta, kuhakikisha sera zinazolinda walaji na wafanyabiashara zinatekelezwa ipasavyo, hususan katika matumizi ya TEHAMA na AI,” amesema  Katambi na kuongeza mkazo  ya  mkazo katika uwekaji wa mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na walaji. 


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa, amesema maadhimisho yalianza kwa shughuli za kijamii, ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu haki zao, umuhimu wa uwazi katika masoko, na namna ya kuepuka vitendo vinavyokandamiza ushindani katika soko.

Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT), Jaji Rose Ebrahim, amewataka wananchi na wafanyabiashara kutoa taarifa za vitendo viovu visivyo vya haki katika soko.

Kwa upande wa  Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani, Dkt. Aggrey Mlimuka amesema  uhusiano kati ya AI na ulinzi wa walaji ni  kuhakikisha uwazi na ufanisi katika biashara.
Naiibu Waziri wa Viwanda na Biashara Patrobas Katambi akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya  Siku Ushindani Duniani,jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Hashil Twaib Abdallah akizungumza kuhusiana wizara itapoendelea kutoa ushirikiano kwa FCC katika kuendeleza ushindani katika soko lenye haki ,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani FCC Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka  akizungumza. 
Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) Jaji Rose Ebrahim akizungumza akitoa maelezo kuhusiana namna ya utatuzi wa migogoro ya wafanyabiashara katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya ushindani  Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa FCC Khadija Ngasongwa akizungumza kuhusiana na umhimu wa maadhimisho ya Siku Ushindani  Duniani katika kuendelea kusimamia ushindani katika soko kati mlaji na wafanyabiashara ,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...