Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Mhe. Christine Grau walipomtembelea leo tarehe 4 Desemba, 2025 katika Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, walizungumza kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha diplomasia ya kibunge (Parliamentary Diplomacy).
Kikao hicho kimehudhuria na Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini Tanzania ambao ni Balozi wa Finland, Balozi wa Hispania, Balozi wa Italia, Balozi wa Ubelgiji na Balozi wa Ujerumani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...