Na WAF – Dar es Salaam.

Serikali imejiwekea malengo makuu ya kitaifa katika kukuza ujenzi wa viwanda vya dawa na kuifanya Tanzania kuwa kinara wa uzalishaji na usambazaji bidhaa za afya barani Afrika.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Desemba 23, 2025 katika kikao cha wazalishaji wa dawa na bidhaa za afya pamoja na uzinduzi wa kikosi kazi cha uharakishaji uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar es Salaam.
”Serikali inatambua wazi kwamba mustakabali wa usalama wa afya ya taifa hauwezi kujengwa kwa kutegemea uagizaji wa dawa pekee, unajengwa kwa kuwezesha wazalishaji wa ndani, kuimarisha uwezo wa viwanda vyetu, na kuviunganisha kikamilifu katika mnyororo wa thamani wa kikanda na kimataifa” amesema Waziri Mchengerwa.

Amesema kupitia uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kutaifanya Tanzania kuwa mzalishaji na msafirishaji mkubwa wa dawa barani Afrika.

“Dira yetu si kuzalisha kwa matumizi ya ndani pekee, bali kuijenga Tanzania kuwa kitovu cha uzalishaji na usafirishaji wa dawa kwa Afrika Mashariki, SADC na bara zima la Afrika” amefafanua Waziri Mchengerwa na kuongezea kuwa uwekezaji huo utaiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa kama nchi inayochangia kikamilifu usalama wa afya wa kikanda na kimataifa.

Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza wakati wa
uzinduzi wa kikosi kazi cha uharakishaji uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo Desemba 23, 2025 Jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV


Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa akizindua kikosi kazi cha uharakishaji uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo Desemba 23, 2025 Jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV






Sehemu ya watumishi na wadau wakimsikiliza
Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa wakati wa uzinduzi wa kikosi kazi cha uharakishaji uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini kilichofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Afya leo Desemba 23, 2025 Jijini Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV

















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...