Na Mwandishi Wetu
TANZANIA imeendelea kuthibitisha ubora wake duniani baada ya kunyakua tuzo kubwa za World Travel Awards ngazi ya Dunia, mara baada ya kung’ara pia katika ngazi ya Mabara.
Ushindi huo unaonesha wazi nafasi ya Tanzania kama kinara wa safari na utalii duniani.
Hafla ya tuzo hizo imefanyika katika Exhibition World Bahrain, Manama—nchi ya kisiwa kilichopo kati ya Saudi Arabia na Qatar.
Katika tuzo hizo, Tanzania imetangazwa tena kuwa Nchi Bora Inayoongoza kwa Safari Duniani (World’s Leading Safari Destination 2025), ikiwa ni mara ya tatu mfululizo baada ya ushindi wa miaka ya 2023 na 2024.
Huo ni uthibitisho kuwa Tanzania bado ni chaguo kuu kwa wapenda safari duniani.
Hifadhi ya Taifa Serengeti imeandika historia kwa kutwaa kwa mara ya kwanza kabisa tuzo ya Hifadhi Bora Zaidi Duniani (World’s Leading National Park 2025).
Ushindi huo unaimarisha sifa ya Serengeti kama moja ya maajabu ya dunia yenye mandhari, wanyamapori na tukio la kipekee la Uhamaji wa Nyumbu (The Great Wildebeest Migration).
Vile vile Kisiwa cha Zanzibar kama eneo bora la mikutano na matukio ya biashara (MICE) la mwaka Duniani.
Tuzo hizo zimepokelewa kwa niaba ya Tanzania na viongozi wakuu wa sekta ya utalii akiwemo Dkt. Hassan Abbas ambaye ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii
• Bw. Ephraim Mafuru – Mkurugenzi Mkuu, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
• Bw. Juma Kuji – Kamishna wa Uhifadhi, TANAPA
Ushindi huo unaakisi nguvu ya utangazaji, uhifadhi na ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, wadau wa utalii na wananchi ukiendelea kuiweka Tanzania kama Tanzania Unforgettable, safari bora zaidi duniani.
Katika kilele cha hafla hiyo Tanzania imetangazwa kuwa mwenyeji wa Grand Final ya World Travel Awards mwaka 2026 tukio kubwa linalowakusanya washindi bora wa dunia kutoka sekta nzima ya utalii katika mabara tofauti
Hiyo ni hatua muhimu inayoongeza hadhi ya Tanzania kimataifa, ikithibitisha uwezo wake katika kuandaa matukio ya kimataifa na kuendelea kuwa kitovu cha utalii duniani.
World Travel Awards (WTA) ni tuzo za kimataifa zinazoenzi ubora katika sekta za usafiri, utalii na ukarimu, maarufu kama “the Oscars of the travel industry.”
Zilianzishwa mwaka 1993 na Graham E. Cooke kwa lengo la kuinua viwango vya huduma na kuhimiza ushindani wa kimataifa katika sekta ya utalii.
Leo, hafla zake zinafanyika katika mabara yote, na kilele chake ni Grand Final, ambapo washindi bora wa dunia hutangazwa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...