Na Hamis Dambaya na Kassim Nyaki, Ngorongoro.
Jamii ya kabila la Wahadzabe ina historia ya kuvutia katika kila nyanja ya maisha yao, watalii mbalimbali wanaotaka kujua hadithi nzuri za kuvutia,kusisimua na kuelimisha kuhusu mila, desturi, utamaduni na historia ya wahadzabe huwatembelea katika makazi yao yaliyopo pembezoni mwa Ziwa Eyasi.
Vilevile kwa mgeni au mtalii yoyote akitembelea Makumbusho ya kisasa ya Ngorongoro Lengai UNESCO Jiopaki (Urithi Geopark Museum) inayosimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Wilayani Karatu basi atapata hadithi nzuri na maelezo ya kutosha kuhusu masuala yote ya kabila hili.
Baada ya wiki mbili zilizopita kuchapisha makala zenye hadithi kuhusu kichwa cha nyani na thamani yake katika ushenga na harusi kwa kabila la wahadzabe pamoja na makala iliyohusu adhabu ya kuchepuka katika kabila hilo, wiki hii tutaangazia utaratibu wa mazishi unavyofanyika katika kabila hilo lililotunza historia ya utamaduni na maisha yake.
Wapo baadhi ya watu wanaamini kuwa Wahadzabe huwa hawafi na badala yake hupotea tu hasa kutokana na maisha yao ya kuishi msituni kwa kula Nyama, mizizi na matunda na kwamba jamii hiyo haina mila ya mazishi kama jamii zingine, laaah hasha !!
Ukweli ni kwamba Wahadzabe hufa kama walivyo binadamu wengine na pia katika maisha yao huamini kuwa mtu akifa huwa ameitwa na Mungu wao (HEPEME) wanayeamini kuwa Mungu huyo anaishi kati jua na mwezi na ndiye huwa anawapa baraka katika maisha yao ya kila siku.
Kwa mujibu wa mzee Shagembe Gambai ambae ni Kiongozi wa kabila la Wahadzabe kutoka katika kijiji cha Eyasi Ngorongoro anaeleza kuwa Mungu wao ni mwenye huruma na baraka na ndio maana mtu akifa katika kabila lao huamini kuwa ameenda kwa Mungu wao anayejulikana kama Ishoko au Hepeme.
Mzee Shagembe anafafanua kuwa Wahadzabe huamini kuwa jua na mwezi ni vitu vyenye nguvu sana na huonesha uwezo wa muumba katika kuwapa chakula chao cha kila siku, ambapo maombi yao makuu kwa Mungu (Hepeme) ni kuomba awajalie mawindo na kuwaepusha na majanga yote, mwisho kifo ambacho ni lazima wakipitie.
Mzee Shagembe anaeleza zaidi kuwa mhadzabe anapofariki mazishi yake hufanyika kwa utaratibu ambao ni tofauti na jamii nyingi ambazo kwa kawaida mwili wa marehemu hufukiwa chini ya ardhi au kuchoma moto.
Kwa kabila la Wahadzabe mtu anapofariki mwili wake huchukuliwa na kulazwa pembezoni mwa nyumba aliyokuwa akiishi wakati wa uhai wake.
Baada ya mwili kulazwa pembezoni mwa Nyumba hiyo, waombolezaji/familia hiyo huenda porini kuwinda mnyama yeyote mkubwa kama Pofu, Pundamilia, Kudu au Swala na wakifanikiwa kuwinda na kumuua mnyama huyo wanampeleka na kumlaza sambamba na mwili wa marehemu ulipo.
Baada ya tukio la kulaza mnyama sambamba na mwili wa marehemu, kambi/familia yote iliyokuwa inaishia katika eneo hilo wanahama kwenda kuishi katika eneo lingine la mbali kwa kipindi cha zaidi mwezi mmoja ili kupisha mwili wa marehemu kwenda kwa Mungu wao ambae wao humuita Ishoko au Hepeme.
Na baada ya muda huo kupita, kambi/familia hurudi katika kambi na kuendelea na shughuli zao za maisha za kila siku na muda huo mwili wa marehemu utakua umekwisha nyakuliwa kwenda kwa Mungu.
Katika kipindi chote cha maombolezo kama ilivyo desturi yao huishi kwa umoja ambao hushirikiana kwa kila jambo katika kuhakikisha familia iliyokumbwa na hali hiyo inapewa faraja na kuenziwa huku wakiamini kuwa kifo ni mpango wa Mungu wao na kila mmoja atakufa na kwenda kuishi maishi mengine mbele ya Hepeme.
Jamii hii ya hadzabe kwa sasa inaheshimika kutokana na kuendelea kuishi katika taratibu za kufuata utamaduni, mila na desturi walizorithi kutoka kwa mababu zao na hakuna mabadiliko yoyote ambayo jamii hiyo inayaafiki pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika mwenendo utandawazi na mabadiliko ya binadamu katika dunia ya sasa.
JASIRI HAACHI ASILI.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...