WATEJA wa Oryx Gas Tanzania zaidi ya milioni moja wameshiriki kwenye kampeni ya "GESI YENTE" kwa kutuma jumbe kupitia kadi ambazo zimewekwa katika mitungi ya gesi huku baadhi ya washindi wamepatikana na kukabidhiwa zawadi.
Miongoni mwa zawadi ambazo zimekabidhiwa kwa washindi ni pamoja na pikipiki, baiskeli, majiko ya gesi ya kupikia, mabegi ya shule na zawadi nyingine mbalimbali.
Akizungumza leo Desemba 1, 2025 wakati wa hafla ya utoaji zawadi, Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni hiyo, Shaban Fundi, amesema kupitia kampeni hiyo wanajivunia wateja wao huku akitoa rai kwa wananchi wasidanganyike kwa kubadilishiwa mitungi kwani kuna baadhi ya mawakala wasiowaaminifu wanawashawishi wateja wa Oryx wanawabadilishia mitungi.
“Ukishautoa mtungi wako wa Oryx haitakuwa rahisi kuupata mtungi mwingine.Hivyo ni vema wakahakikishia mtungi wako wa Oryx unabakia nao mwenyewe.”
Kuhusu kampeni ya GESI YENTE amesema kampeni hiyo ilianza Agosti 13 mwaka huu wa 2025 na ilikuwa ya miezi mitatu lakini kutokana na maombi ya mawakala kuwa iendelee hivyo wameisogeza mbele hadi Desemba 15 mwaka huu,hivyo ametoa rai kwa wateja kuendelea kushiriki ili kujishindia zawadi mbalimbali.
“Tangu tulipozindua kampeni hii ya GESI YENTE yenye lengo la kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia mwitikio mkubwa umekuwa mkubwa sana,tumefikia wateja wengi,tumeshuhudia wateja wa Oryx wakituma jumbe mbalimbali kupitia maelezo tuliyoweka katika kadi zilizipo katika mitungi yetu ya gesi.”
Aidha amewahakikishia Watanzania kuwa wataendelea kuboresha huduma zao kwa kuboresha miundombinu, kupanua mtandao wa usambazaji, ili kutekeleza ajenda ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa ajili ya afya bora, mazingira safi, na maendeleo endelevu.
Kwa upande wa wateja ambao wameshinda zawadi za majiko ya Oryx,baiskeli ,pikipiki na mabegi ya shule wameipongeza kampuni hiyo kwa kuwa na kampeni maalum yenye lengo la kuhamasisha jamii ya Watanzania kutumia nishati safi ya kupikia na kuachana na matumizi ya kuni na mkaa.
Irene Godfrey ambaye ni mkazi wa Mbezi Beach Dar es Salaam aliyeshinda zawadi ya pikipiki amesema kampeni ya GESI YENTE imemuwezesha kumpatia mtaji kwani pikipiki hiyo ataitumia kwa shughuli mbalimbali za uzalishahi huku akisisitiza matumizi ya gesi ya kupikia ndio mkombozi wa afya na mazingira.
Kwa upande wake Elikana Madirisha amesema kuwa kupata jiko la Oryx kwake inakwenda kurahisisha katika kuandaa chakula kwani kupiga kwa gesi kunarahisisha muda wa kukaa jikoni na muda mwingi kutumika katika kufanya maendeleo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...