Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, wameitembelea Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” iliyokita kambi jijini Cairo nchini Misri. 

Waziri Kombo na Profesa Kabudi, wameitembelea kambi hiyo Desemba 17, 2025 na kuikabidhi bendera ya Taifa, ikiwa ni ishara ya kuitakia kila la kheri na kuitia shime kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha michuano ya Kombe la AFCON huko nchini Morocco kinachotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwaka huu. 

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Balozi Kombo amewasihi vijana hao wachache kati ya wengi wa taifa hili kwa kutanguliza uzalendo kwanza na kuipigania bendera ya Taifa kwa jasho na damu ili kuliletea heshima taifa la Tanzania.

Kwa upande wake, Mhe. Prof. Kabudi, amekiahidi kikosi hicho ushirikiano wa kila aina katika kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vyema katika michuano hiyo mikubwa na yenye heshima kubwa sio tu barani Afrika bali duniani kwa ujumla.

Aidha, Prof. Kabudi amewahimiza Watanzania kuipenda na kuipa moyo timu yao ya Stars kwa kuwashangilia na wale watakao kuwa na nafasi kwenda kujiunga nao kwenye mechi zao zote watakazocheza huko nchini Morocco.

Ikumbukwe kwamba kikosi cha Taifa Stars kipo kundi C lenye timu za Nigeria, Tunisia na Morocco na kikosi hicho kitaanza michuano hiyo kwa kucheza na moja ya timu bora barani Afrika timu ya Taifa ya Nigeria.








Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...