-Ataka Maafisa hao kuwa na takwimu sahihi za vijana

-Kuunganisha vijana na programu na fursa za Ujuzi, Ajira na Uwezeshaji Kiuchumi

Na: Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana – Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka ametoa maagizo manne (4) kwa Maafisa Maendeleo ya Vijana wa Mikoa na Halmashauri kwa lengo la kuboresha na kuimarisha ustawi wa vijana na Maendeleo yao nchini.

Aidha, Mhe. Nanauka amewataka maafisa hao, katika kutekeleza majukumu yao wahakikishe wanakuwa na takwimu sahihi za vijana waliopo katika maeneo yao na waweze kutambua changamoto zinazowakabili vijana na kutafuta ufumbuzi. Pili, kuwaunganisha vijana hao na programu na fursa zote za kitaifa zinazohusu ujuzi, ajira na uwezeshaji wa kiuchumi.

Vile vile, amewataka Maafisa Maendeleo ya Vijana kuimarisha ushirikiano na wadau waliopo katika Mikoa na halmashauri zenu ili kuleta matokeo ya haraka na endelevu kwa vijana pamoja na kuzingatia uwajibikaji, uadilifu na matumizi sahihi ya rasilimali zinazotolewa kwa ajili ya vijana.

Amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa Maendeleo ya vijana wa mikoa na halmashauri kilichofanyika ukumbi wa Hazina, leo Disemba 17, 2025, Jijini Dodoma.

Waziri Nanauka amesema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imechukua hatua za kimkakati za kuimarisha mifumo ya sera, sheria na utendaji kuhusu maendeleo ya vijana na hivyo kupelekea kuanzishwa Wizara yenye dhamana mahsusi ya Maendeleo ya Vijana chini ya Ofisi ya Rais.

Kwa upande mwengine, Waziri Nanauka ametoa rai kwa Maafisa Maendeleo ya vijana kuzingatia falsafa tatu (3) za wizara hiyo ambayo ni, Kasi ya kusikiliza na kutekeleza mawazo na ushauri wa vijana, Kuwafikia vijana walipo na kuwasikiliza na Kutumia teknolojia ili kwenda na kasi ya vijana.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...