-Pia azungumzia nguvu ya wanachama walioko katika mashina,matawi
-Asisitiza nafasi ya wazee katika kutoa elimu ya itikadi kwa vijana
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.Asha-Rose Migiro amesema kuna kila sababu ya kuhakikisha Chama hicho kinazingatia utaratibu wa kusikiliza maoni na ushauri kuanzia ngazi ya chini badala ya utaratibu wa maelekezo kutoka juu kwenda chini.
Akizungumza mbele ya mamia ya mabalozi wa mashina wa Wilaya za Temeke na Kigamboni katika kikao kazi kilichofanyika ukumbi wa PTA uliopo Sabasaba jijini Dar es Salaam,Dk.Migiro ametumia kikao hicho kutoa rai kwa viongozi na wana CCM kuzingatia utaratibu wa kutoa maoni kuanzia ngazi ya chini kwenda juu.
“Nitoe mwito kwa viongozi wetu tusifanye utaratibu wa kutoa amri kutoka juu kushuka chini maana uongozi mzuri ni lazima uanzie chini kwenda juu.Yale tunayoyapata kutoka kwenye mashina , matawi ndio yatapanda juu kwa lengo la kukiimarisha chama chetu.
“Tusikilize kutoka chini kupanda juu tusiwe wa kutoa amri kutoka juu kwenda chini na hiyo ni kazi yetu wanachama wote wa CCM , viongozi wetu mlioko katika mashina,mimi katibu mkuu pamoja na viongozi wote wa Sekretarieti tunapenda kuona hili linafanyika .
“Kwasababu sisi amri yetu inatoka chini,hivyo niwaombe ndugu zangu wa mashina, matawi na kata muwe huru wakati wowote kuniletea ujumbe au taarifa ya namna ambavyo tutaweza kukiimarisha chama chetu kwenye ngazi hii ya matawi ni muhimu sana.”
Dk.Migiro amesema katika kipindi hiki wamekubaliana ndani ya Sekretarieti kwamba Katibu Mkuu atakapoanza ziara zake waanze kwenye ngazi za mashina, matawi na kata kwa lengo la kuangalia umadhubuti na uimara wa chama chao unapoanzia.
“Na Mwenyekiti wetu Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wetu azma yake ni kuhakikisha Chama hiki kinapata uimara siku hadi siku na yeye ni mojawapo ya viongozi wetu,yeye akiongoza viongozi wengine amekuwa akisisitiza umadhuti wa mashina matawi na kata.
“Tunapokwenda kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi tunawajibu wa kurejea mambo mazuri ambayo tumekuwa tukiyafanya katika chama cha Mapinduzi.Wakati sisi ni chipukizi ,vijana na tukaenda UWT tukaingia chama tulikuwa tunakwenda kwa ngazi…
“Na tulikuwa tunapata madarasa ya itikadi kutoka ngazi za chini kabisa , ambayo yalitufundisha tumetoka wapi ,tunakwenda wapi,ni namna gani tunajenga kada ya viongozi ambao wameishiba vizuri itikadi ya chama cha Mapinduzi.Hivyo kuna kila sababu ya kurithisha itikadi za chama chetu kwa vijana.”
Wakati huo huo amezungumzia umuhimu wa chama hicho kuendelea kuwatumia wazee kwani ni hazina ya chama ambayo inaweza kutumika vizuri.”Tuwatumie wazee hawa katika kutoa madarasa ya itikadi,wao wanajua misingi ya chama chetu.Tuwe karibu na viongozi wenzangu tuwatumie wazee hawa katika kujenga Chama Cha Mapinduzi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...