Na Mwandishi wetu, Babati


MBUNGE wa Jimbo la Babati Mjini, Mkoani Manyara, Emmanuel Khambay amewataka maofisa ardhi wa Halmashauri ya Mji huo kufanya kliniki ya ardhi kwenye kata ili kuondoa migogoro ya ardhi inayowakabili baadhi ya wananchi.

Khambay ametoa agizo hilo kwenye kata ya Maisaka katika ziara ya kushukuru kwa kuchaguliwa na kusikiliza kero, malalamiko na changamoto zinazowakabili wakazi wa eneo hilo.

Ameeleza kwamba miongoni mwa malalamiko, kero na changamoto alizozipata katika jamii ni migogoro ya ardhi kwenye kata ya Maisaka hivyo maofisa ardhi waanzishe kliniki katika eeo hilo.

"Maofisa ardhi wa halmashauri anzisheni kliniki ya ardhi na kukutana na wakazi wa kata ya Maisaka, msikilize changamoto zao na kuwapatia majawabu," amesema Khambay.

"Lengo la ziara hii ni kuwashukuru na kusema asante kwa kunichagua na kusikiliza kero mbalimbali na miongoni mwa changamoto nilizozisikia ni migogoro ya ardhi," amesema Khambay.

Amesema tiba ya migogoro ya ardhi ni kuanzisha kliniki ya ardhi kwa maofisa ardhi kutoka ofisini na kwenda kwa watu kusikiliza matatizo yao na kueleza namna ya kuyatatua.

Hata hivyo, amewaahidi wakazi wa eneo hilo, kuendelea kushirikiana nao kufanikisha maendeleo na kutoa huduma bora bila upendeleo wowote ule.

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Babati mjini, Elizabeth Malley amempongeza Khambay kwa kushika nafasi hiyo na kujitoa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa mjini Babati.

Malley anewaomba wakazi wa Babati mjini wampe ushirikiano wa kutosha mbunge wao ili aweze kuwatumikia ipasavyo kwani uchaguzi umeshafanyika na kilichobaki ni kufanyika maendeleo.

Mmoja kati ya wakazi wa kata ya Maisaka, Rose John amepongeza hatua hiyo ya kufanyika kwa kliniki ya ardhi itakayofanywa na maofisa ardhi wa halmashauri hiyo.

Amesema kupitia kliniki hiyo itakayofanywa wataweza kumaliza migogoro ya ardhi ambayo kwa namna moja au nyingine inazorotesha maendeleo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...