Na Kassim Nyaki, Arusha.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) leo tarehe 29 Januari, 2026 jijini Arusha amezindua bodi ya wakurugenzi wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na kuielekeza kusimamia uhifadhi, kubuni mazao mapya ya utalii na kuyatangaza na kuboresha huduma za maendeleo kwa wananchi wa  wilaya ya Ngorongoro.

Dkt. Kijaji amebainisha kuwa hifadhi ya Ngorongoro ni eneo muhimu kiuhifadhi na moja ya maeneo yanayotambuliwa kama urithi wa dunia na UNESCO hivyo  ameiunda bodi hiyo kwa kuteua manguli wa kila sekta ili kufikia matamanio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, Samia Suluhu Hassan ya kuona uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii vinasimamiwa bila kuipoteza hifadhi hiyo.

“Nimeteua wataalam kutoka sekta zote serikali na binafsi  ili muisaidie serikali katika kusimamia maeneo hayo kwani hifadhi ya Ngorongoro ina mvuto mkubwa duniani,hivyo ni jukumu lenu kutumia taaluma na weledi wenu katika kuhakikisha Ngorongoro inaendelea kuwa na tija kwa taifa”,alisema Waziri Kijaji.

Ubobezi wa wakurugenzi wapya wa bodi ya Ngorongoro  na umahiri wao kitaaluma ulielezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Hassan Abbasi ambaye alisema kazi ya kuwateua wakurugenzi hao wa bodi haikuwa rahisi kutokana na uchambuzi yakinifu uliofanywa ili kupata watu ambao watakuwa msaada kwa hifadhi  hiyo na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya  Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro ambae ni Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali Venance Mabeyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kumteua tena kuongoza bodi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu   na kumpongeza waziri wa  Maliasili na Utalii kwa kuteua watu wenye taaluma  tofauti  na kuwataka  wakurugenzi hao kuacha alama kama ilivyokuwakwa  wakurugenzi wa bodi iliyopita.

Wakurugenzi wapya wa bodi wa mamlaka hiyo wamebobea katika sekta ya uhifadhi, utalii, fedha na uchumi, utawala, sheria, diplomasia,utawala bora, maendeleo ya jamii, ukaguzi na teknolojia  ya mifumo ambapo pia wana uzoefu mkubwa katika utumishi wa serikali na sekta binafsi hivyo kutoa mwanga wa kutosha katika kuimarisha mamlaka hiyo.

Mapema Kamishna wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro bwana Abdul-Razaq Badru alivishwa cheo na kuapishwa rasmi kuwa kamishna wa mamlaka hiyo na kuahidi kuendelea kuchapa kazi kwa weledi  na uaminifu wa hali ya juu ili kuimarisha majukumu ya Ngorongoro ambayo ni uhifadhi, utalii na maendeleo ya jamii.

 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...