Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya Marekani katika matumizi ya teknolojia na vifaa vya kisasa ili kutafsiri kwa ufanisi taarifa za utafiti katika sekta ya madini, hususan madini ya kinywe (graphite).
Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 21, 2026, Mhe. Mavunde amesema Wizara ya Nishati na Madini ya Serikali ya Marekani Watatoa mafunzo kwa Wataalamu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) pamoja na Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) kupitia programu ya kuwajengea uwezo na ujuzi wataalamu wa sekta ya madini kupitia mafunzo ya siku mbili yanayotarajiwa kutolewa.
Amesema kupitia ushirikiano huo, Tanzania itaongeza maeneo ya nchi yaliyofanyiwa utafiti wa kina wa madini, na iko tayari kushirikiana na nchi mbalimbali, ikiwemo Marekani, katika shughuli za utafiti wa rasilimali hizo.
Mhe. Mavunde ameongeza kuwa maeneo yatakayofanyiwa utafiti ni pamoja na leseni zinazotolewa na STAMICO, ambapo utafiti wa pamoja utafanyika ili kubaini maeneo yenye rasilimali nyingi za madini, hatua itakayosaidia kuanzisha migodi mikubwa, hususan katika mikoa ya Mtwara na Lindi.
Amebainisha kuwa kufikia mwaka 2050, mahitaji ya madini ya kinywe yanatarajiwa kufikia tani milioni 4.5 kwa mwaka, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zilizo katika nafasi nzuri ya kuwa msambazaji muhimu wa madini hayo duniani.
Aidha, ameeleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofahamika kuwa na utajiri wa madini mbalimbali, jambo linaloifanya Marekani kuja na programu ya kuisaidia sekta ya madini nchini, ikizingatiwa kuwa nchi hizi mbili zimekuwa na uhusiano mzuri wa muda mrefu.
Kwa upande wake, Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Andrew Lentz, amesema Marekani ina furaha kubwa kwa ushirikiano mzuri unaotolewa na Tanzania katika utekelezaji wa mradi huo muhimu, unaolenga kuwanufaisha wananchi wa pande zote mbili, na ameonesha matarajio ya kuendeleza zaidi ushirikiano huo.
Ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani katika utafiti wa madini ya kinywe utaimarisha sekta ya madini kupitia utafiti wa kina, ujenzi wa uwezo wa wataalamu na kuvutia uwekezaji, hatua itakayoiwezesha Tanzania kunufaika na ongezeko la mahitaji ya madini hayo duniani.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...