Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeanza utekelezaji kwa vitendo wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuwekeza kwenye sayansi na teknolojia, baada ya kuwaaga wanafunzi 16 waliopata ufadhili wa masomo ya juu nje ya nchi kupitia mpango wa 'Samia Scholarship'
Wanafunzi hao wanaelekea katika Chuo Kikuu cha Johannesburg nchini Afrika Kusini kwa masomo yanayolenga kuzalisha wataalamu bingwa katika sayansi ya data, akili unde (Artificial Intelligence – AI) na teknolojia ya viwandani.
Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao Januari 30, 2026, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema ufadhili huo unalenga kuongeza idadi ya wataalamu katika maeneo ya sayansi ya data, akili unde na teknolojia ya viwanda.
“Mnakwenda Afrika Kusini kwa ufadhili wa masomo ambayo Rais Samia alituagiza nasi tunatekeleza kupitia wanafunzi hawa 16 kati ya 50 waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita kwenye masomo ya sayansi yanayojumuisha hisabati ya juu (Advanced Mathematics),” amesema Prof. Mkenda.
Ameongeza kuwa wanafunzi hao wametoka katika shule mbalimbali zikiwemo shule za serikali, akieleza kuwa kati ya wanafunzi 50 waliochaguliwa, 16 wanaanza masomo Chuo Kikuu cha Johannesburg huku 34 wakitarajiwa kuendelea na masomo katika vyuo vikuu vya Ireland.
Prof. Mkenda amesema wanafunzi hao watanufaika na masomo ya darasani pamoja na kuunganishwa na kampuni za kiteknolojia zilizopo nchini Afrika Kusini ili kuwajengea uzoefu wa vitendo.
Amesema serikali imeahidi kuwekeza kwenye sayansi kwa lengo la kuzalisha wataalamu katika teknolojia ya tehama, sayansi ya data, akili unde, sayansi ya kompyuta na teknolojia ya viwandani.
“Adhima yetu ni kuongeza wanasayansi wabobezi katika maeneo hayo. Tutatumia mfuko wa Samia Scholarship kuwasomesha wanasayansi ili kuwafanya wabobezi ndani na nje ya nchi,” amesema.
Ameeleza kuwa serikali itaendelea kutoa ufadhili kwa wanafunzi wanaofanya vizuri katika masomo ya sayansi ili kukidhi mahitaji ya taifa katika sekta mbalimbali.
Prof. Mkenda amesema Tanzania imekuwa na uhaba mkubwa wa wataalamu wa Sayansi ya Nyuklia licha ya kuwa na madini ya urani, hali inayozuia nchi kunufaika kikamilifu na rasilimali hiyo.
“Sayansi ya nyuklia ni muhimu katika tiba, kilimo, maendeleo ya teknolojia na maeneo mengine. Ndiyo maana tumeanza kupeleka Watanzania kusoma shahada ya pili katika masuala ya sayansi ya nyuklia kupitia Tume ya Nguvu za Atomi Tanzania,” amesema.
Ameongeza kuwa kwa shahada ya kwanza, serikali inachukua wanafunzi waliofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi na hesabu baada ya kumaliza kidato cha sita na kuwapeleka kusoma nje ya nchi.
Amesema kwa sasa wameanza na wanafunzi 50, ambapo baadhi wanasoma nje ya nchi na wengine wanapata ufadhili wa kusoma ndani ya nchi, akisisitiza kuwa programu hiyo inatekelezwa kwa haki na uwazi bila upendeleo.
“Hatuchagui kwa sura, tunaangalia ufaulu. Kigezo kikuu ni kufanya vizuri kitaaluma. Ninyi ni wababe ndiyo maana mmechaguliwa,” alisisitiza Prof. Mkenda.
Pia amesema serikali imeweka fedha za kuwasomesha Watanzania shahada ya pili katika vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo Nelson Mandela Institute of Science and Technology pamoja na Chuo Kikuu cha India chenye tawi Zanzibar.
Ametoa wito kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kuweka jitihada za makusudi katika masomo ya sayansi.
“Katika hili hakuna ujanja ujanja. Haijalishi wewe ni mtoto wa nani, ukifaulu vizuri tunaorodhesha kuanzia wa kwanza mpaka bajeti itakapoisha,” amesema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Carolyne Nombo amesema uwepo wa wanafunzi hao ni ushahidi wa dhamira ya serikali ya awamu ya sita katika kuendeleza elimu ya sayansi na teknolojia.
“Kuwepo kwenu hapa leo ni ushahidi wa wazi wa dhamira ya serikali katika kuwekeza kwenye sekta ya elimu hususan sayansi na teknolojia,” amesema Prof. Nombo.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Sayansi, Dk. Amos Nungu amesema ufadhili huo utachochea maendeleo ya sayansi na teknolojia hususani katika eneo la akili unde na kutoa mtazamo mpya wa maendeleo ya sayansi nchini.
Miongoni mwa wanufaika wa ufadhili huo, Malaika Florence amesema safari yao imekuwa ndefu tangu kidato cha sita ambapo walikuwa wanafunzi 50 wa kwanza kitaifa kabla ya kuandaliwa katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela.
“Tumejengewa uwezo na misingi mbalimbali ikiwemo mafunzo ya kompyuta, usimamizi wa fedha na maarifa ya kuijua dunia,” amesema.
Ameongeza,“Tunalijua taifa limetuamini. Tunaahidi kusoma kwa bidii ili tuwe sehemu ya kutimiza malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050,” amesema.
Naye Simon Asilwe amesema utayari wa serikali kwao ni deni ambalo watalilipa kwa kurejesha matunda ya utaalamu watakaoupata kupitia ufadhili huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...