WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso, amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kufanya tathmini ya kina ya watendaji ndani ya wizara na taasisi zake na kuwaondoa wale wote "wanaohudhuria" kazini bila kuleta matokeo chanya ya wananchi kunywa maji.
Waziri Aweso alitoa kauli hiyo jana wilayani Mkinga wakati wa hafla ya kukagua na kupokea vifaa vya mabomba yenye thamani ya shilingi Bilioni 7.7, kwa ajili ya umaliziaji wa mradi wa maji wa Mkinga-Horohoro ambao sasa umefikia asilimia 65 ya utekelezaji wake.
Akizungumza kwa msisitizo, Waziri Aweso alisema tangu kuteuliwa kwake tena kuongoza wizara hiyo, amekuwa haridhishwi na namna baadhi ya watendaji wanavyotekeleza majukumu yao, akibainisha kuwa wizara inahitaji watendaji wanaopambana kukamilisha miradi na si wale wanaokwamisha huduma.
"Wizara ya maji hatutaki watu wanaohudhuria kazini, tunataka watendaji wanaoleta matokeo. Unakuwa mtendaji miaka mitano hujaenda hata kuzindua kisima kimoja? Haiwezekani. Lazima watendaji mkae mkijua kuwa wananchi wanajenga chuki na Serikali yao kwa sababu ya watumishi wasiotekeleza wajibu wao," alionya Waziri Aweso.
Aliongeza kuwa faraja ya mhandisi yeyote wa maji ni kuona wananchi wanapata huduma, na endapo hilo halifanyiki inaleta ukakasi kwa Wizara na Serikali kwa ujumla.
Katika hatua nyingine, Aweso amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Mwajuma Waziri, kuhakikisha miradi viporo takribani 1,000 iliyoanzishwa nchini inakamilika haraka. Alitolea mfano wilaya ya Mkinga pekee ambayo ina miradi mitano inayohitaji kukamilishwa.
"Katibu Mkuu, nenda kafanye tathmini... wale wanaohudhuria kazini bila kufanya kazi tuwaondoe. Kama tumeweza kumaliza mradi mgumu wa Same-Mwanga, kwanini miradi mingine isua-sue? Twendeni tukafanye kazi, nami nipo tayari unipangie ziara ya kuzindua miradi na si kukagua mabomba pekee," alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga UWASA, Mhandisi Geofray Hilly, alibainisha kuwa mradi huo wa Mkinga-Horohoro wenye thamani ya shilingi Bilioni 35, unakwenda kunufaisha wananchi 57,000 waliopo katika vijiji 37.
Katibu Mkuu, Mhandisi Mwajuma Waziri, alimhakikishia Waziri kuwa ameshamuelekeza mkandarasi kuongeza nguvu kazi ili mradi huo ukamilike ifikapo Julai mwaka huu, huku Mbunge wa Jimbo la Mkinga, Twaha Mwakioja, akishukuru kwa hatua hiyo akisema ni mkombozi dhidi ya adha ya kufuata maji umbali mrefu.
Waziri Aweso alihitimisha kwa kusema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa fedha nyingi katika sekta ya maji, hivyo ni wajibu wa watendaji kuunga mkono juhudi hizo kwa uadilifu na kasi ya matokeo.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...