Na. Mwandishi wetu – DSM

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano Mhe. Deus Clement Sangu (Mb.) ametembelea Ofisi za Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Makao Makuu Januari 03, 2025 Jijini Dar es Salaam na kukutana na Viongozi kwa lengo la kujitambulisha na kulitambulisha jukumu jipya la Mahusiano ambalo Ofisi yake imekabidhiwa kuliratibu. 

Aidha, Waziri Sangu alipowasili amepokelewa na Mufti na Mwenyekiti wa BAKWATA, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally, pamoja na wajumbe wa Baraza hilo. 
Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Sangu alipongeza Baraza hilo kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha amani, umoja na mshikamano nchini. 

Vilevile, alieleza kuwa BAKWATA imekuwa nguzo muhimu ya maadili na mshikamano wa kijamii kwa kuhimiza mazungumzo ya amani, kuvumiliana na kuimarisha mahusiano mema baina ya waumini wa dini mbalimbali. 

“Juhudi hizo zimechangia kwa kiasi kikubwa kudumisha utulivu na mshikamano wa kitaifa” amesema.

Aidha, Mhe. Sangu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na taasisi za kidini katika kushughulikia changamoto za kijamii, kiuchumi, kisiasa, kikanda   na kimataifa hususan malezi bora na maadili mema katika jamii. 

Sambamba na hayo, ameihakikishia BAKWATA kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na Baraza hilo na taasisi mbalimbali kuendeleza agenda ya amani, mshikamano na maendeleo jumuishi.
Kwa upande wake Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally,  amempongeza Rais kwa kutambua  umuhimu wa Mahusiano na kuazisha Wizara mahsusi  inayoshughulikia mahusiano.

Aidha, ameishukuru Serikali kwa kutambua na kuthamini mchango wa Baraza na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuimarisha umoja wa kitaifa, amani na mshikamo.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...