Na Seif Mangwangi, Michuzi TV Arusha
TANZANIA inaelezwa kuwa na utajiri wa miundombinu ya barabara wenye thamani ya zaidi ya Sh.trilioni 38 hivyo kazi kubwa ya Serikali ni kuhakikisha inalinda miundombinu hiyo kwa kuzifanyia ukarabati wa kila mara.
Hayo yameelezwa leo 9 Januari 2026, Jijini Arusha na Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega wakati wa ufunguzi wa mkutano wa chama cha mifuko ya matengenezo ya Barabara Afrika(ARMFA).
Aidha mkutano huo umetumika kumsimika Rais mpya wa chama hicho Mtanzania, Mhandisi Rashid kambanga ambaye ataongoza chama hicho kwa miaka miwili.
Ulega amesema chama hicho kimekuwa mhimili mkuu wa kuhakikisha barabara zinazotengenezwa zinatunzwa kwa kufanyiwa ukarabati wa mara kwa mara kwa kuwa zimekuwa zikitumika fedha nyingi kwenye ujenzi.
Amesema asilimia themanini ya usafiri nchini umekuwa ukitegemea miundo mbinu ya barabara hivyo ni jukumu la Serikali kuhakikisha kila wakati miundo mbinu hiyo inakuwa salama Ili kuendeleza shughuli za kiuchumi.
“ Hizi Barabara kuwa nazo ni jambo moja lakini kuzitunza ni jambo lingine, sasa hii bodi kazi yake kubwa ni pamoja na kuzitunza hizi barabara, na ndio sababu nchi za Afrika kupitia Kwa wataalam wake wakaamua kuuanda hiki chombo,” amesema.
Waziri Ulega amesema Tanzania na nchi sita zinazoizunguka ni wanufaikaji wakuu wa chama hicho kutokana na kuwa na matumizi makubwa ya barabara kutokana na uwepo wa bandari ambapo nchi hizo hupitisha mizigo yake.
“ Nchi za Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Zambia, Malawi, Uganda, Burundi, Rwanda, zote zinategemea bandari yetu, uchumi wao inategemea barabara kwa kupitisha mizigo, Kwa hiyo ni muhimu sana kukarabati barabara,” amesema.
Rais mpya aliyekabidhiwa wadhifa huo ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa mfuko wa barabara nchini, Mhandisi Rashid Kambaga amesema mfuko wa barabara umekuwa na umuhimu mkubwa kwa kuwa unaisaidia Serikali kutunza miundombinu hiyo.
“ Serikali kwa kawaida ina mambo mengi sana, ukisema ijenge barabara na bado ikarabati itashindwa kutekeleza mambo mengine kwa hiyo mfuko huu unasaidia kutunza miundombinu hii katika nchi,” amesema.
Amesema umoja huo ni kuhakikisha wanashirikiana na wanabadilishana uzoefu wa namna ambavyo wamekuwa wakitekeleza jukumu la kutunza barabara katika nchi zao ikiwemo upatikanaji wa fedha.
“ Nchi nyingi huwa tunakosa rasilimali fedha kwaajili ya kukarabati barabara zetu, kwa hiyo huwa tunabadilishana uzoefu wa kujua wenzetu wamefanyaje lakini pia kujua chanzo kizuri cha kupata fedha na sisi tunaishauri Serikali zetu,” amesema.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...