Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameitaka wizara ya maji kuchukua hatua za kisheria kwa yeyote atakayebainika kuchezea vyanzo na miundombinu ya kwani ni sawa na kuchezea na uhai.
Ameyasema hayo jana wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya Mkutano wa Bodi za wakurugenzi wa Mamlaka za maji safi na Usafi wa mazingira nchini kilichofanyika Mkoani Arusha katika hotel ya Ngurdoto ambapo amesisitiza utumiaji mzuri wa maji ili kuepusha malalamiko.
"Jana nimepata taarifa ya watukukata mabomba ya maji na kutengeneza urembo chukueni hatua Kali za kisheria , pia nisisitize sitaki kuona mwanafunzi amebeba Kidumu cha maji, Shule za misingi, Secondary, Hospitali, Vituo vy Afya, zahanati zote ziwe na visiima vya maji" Alisema Dkr Mwigulu.
Waziri Mkuu anesema Jambo hilo la kutunza vyanzo na miundombinu ya maji siyo kazi ya Wizara ya Maliasili na Utalii pekee bali ni kwa watanzana wote, kwani ni mihimu kuzingatia matumizi sahihi ya maji, "Fungulia unapotumia funga unapomaliza kutumia
Awali akitoa salami za Wizara Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia katika kipindi cha miaka 4 zaidi ya trilion 3 zimeongezwa katika miradi ya maji mjini na vijijini ambapo vijijini imefika asilimia 85.2% kwa eneo la mjini asilimia 92.5 ,ipo miradi ya miezi 28 inayoendelea kuvuka lengo la asilimia 95℅ kwa mjini wana miradi zaidi ya 878 inaendelea
Amesema mpaka sasa wana vijiji takribani 12333 kupitia wakala wa maji vijijini RUWASA wameshafikia vijiji 10,758 wamebakisha vijiji 1575 hadi kufikia 2030 vyote vitakuwa vimepata huduma ya maji safi na salama
"Tumeanzisha Bodi za Mamlaka za maji majukumu lake ni kusimamia Mamlaka. hizo zilete ufanisi na kuhakikisha huduma mwananchi ataipata inakuwa bora na haina malalamiko ya aina yeyote Sisi katika Wizara hii tunakuhakikishia kwenda kufanya kazi zenye matokeo"
Amemuomba Waziri mkuu kuangakia ongezeko la bajeti ya Wizara ya maji huku akitilia mkazo Wizara hiyo imejiwekea malengo makuu 3 ikiwemo kuleta matokeo chanya katika utendaji, mifumo na teknolojia kwa kushirikiana na chup cha maji ili kuleta ufanisi katika taasisi mageuzi makubwa, pamoja na teknolojiaa italayotumika kuleta mageuzi chanya kwenye sekta za maji.
"Ni aibu Leo hii mwananchi alalamike amebambikiwa bili za maji hapana,haya ni maelekezo ya Rais kwamba tunakwenda kwenye mita janja muta kama luku ya umeme ili kuhakikisha tunaondokana na malalamiko" Alisema
Dkt James Andilile ni mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) amesema maisha ya kila siku ya mtanzania yanaanza na maji hivyo wanalo jukumu la. Kuhakikisha uwekezaji mkubwa ambao umefanywa na serikali unaleta tija kwa huduma ya maji safi na salama.
"Tunaendelea kufuatilia na kuhakikisha kwamba Mamlaka za maji zinatoa huduma kama inavyotakiwa pia zinatekeleza na lengo namadhumuni ya serikali"
Sambamba na hilo Dkt. Mwigulu akizindua Mfumo wa kuunganisha maji kwa njia ya mtandao,( b) Uzinduzi wa mkakati wa kuanzishwa ufungaji wa mita za maji ya malipo ya kabla, (c) mkakati , aidha ufungaji wa mita za maji za malipo ya kabla kwa mwaka 2024 ziliungwa mita13528 hadi kufikia 2026 januari zimefungwa mita 23156








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...