Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC Bi. Khadija Ngasongwa, akitoa maelezo kuhusu wajibu wa FCC kwenye kusimamia ushindani na kumlinda mlaji wakati wa kikao kazi na wazalishaji wa saruji nchini kilichofanyika katika ofisi za FCC Februari 11, 2026 Jijini Dar es Salaam.
.............
TUME ya Ushindani (FCC) imekutana na wadau wa uzalishaji wa ndani wa saruji kwa lengo la kujadili hali ya uzalishaji wa bidhaa hiyo pamoja na namna ya kulinda soko na maslahi ya mlaji.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bi. Khadija Ngasongwa, amesema kuwa tume hiyo ina utaratibu wa kukutana na wadau wake mara kwa mara ili kujadili masuala yanayohusu ushindani wa soko.
Amesema kikao cha leo kimewaleta pamoja wazalishaji wa saruji kwa ajili ya mahojiano na majadiliano yatakayosaidia kujenga soko lenye ushindani wa haki sambamba na kumlinda mlaji.
Bi. Ngasongwa amesema baada ya majadiliano hayo, FCC itapata mwanga wa kuchambua na kutoa mwelekeo au suluhisho kuhusu hali ya ushindani wa saruji sokoni na athari zake kwa walaji.
Aidha, amesema wazalishaji wa saruji waliwasilisha taarifa (notice) ya kupandisha bei ya bidhaa hiyo, jambo linalohitaji kufanyiwa tathmini ya kina kwa kuzingatia hali halisi ya soko, gharama za uendeshaji pamoja na gharama za malighafi.
“Katika majadiliano haya, tunatarajia kupata matokeo yatakayojenga afya ya soko la saruji na kuhakikisha mlaji analindwa katika upatikanaji wa bidhaa hii muhimu,” amesema Bi. Ngasongwa.
Kikao hicho kimefanyika Februari 11 katika ofisi za FCC, Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC Bi. Khadija Ngasongwa, akitoa maelezo kuhusu wajibu wa FCC kwenye kusimamia ushindani na kumlinda mlaji wakati wa kikao kazi na wazalishaji wa saruji nchini kilichofanyika katika ofisi za FCC Februari 11, 2026 Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu FCC Bi. Khadija Ngasongwa, akitoa maelezo kuhusu wajibu wa FCC kwenye kusimamia ushindani na kumlinda mlaji wakati wa kikao kazi na wazalishaji wa saruji nchini kilichofanyika katika ofisi za FCC Februari 11, 2026 Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wazalishaji wa saruji wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bi. Khadija Ngasongwa akizungumza wakati wa kikao kazi cha wazalishaji wa saruji Februari 11, 2026 jijini Dar es Salaam.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...