Na Mwandishi Wetu,Zanzibar

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Mhe. Suleiman Masoud Makame, amelishukuru Wakala wa Kimataifa wa Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) kwa namna shirika hilo linavyoisaidia Zanzibar katika sekta ya kilimo na mifugo.

Akizungumza katika ofisi za Wizara ya Kilimo Zanzibar baada ya kupokea ugeni kutoka IAEA, ugeni ulioongozwa na Bwana Gashaw Gebeyehu Wolde, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kiufundi kwa Afrika, pamoja na Bi. Azza Kashlan, Afisa wa Usimamizi wa Programu, Waziri Makame alisema wizara yake itaendelea kushirikiana kwa karibu na IAEA ili kuhakikisha ushirikiano huo unaimarika zaidi, kama ambavyo umefanikiwa katika maeneo ya mazao na mifugo.

Kwa upande wake, Bwana Gashaw Gebeyehu Wolde alisema kuwa IAEA ina miradi ya kitaifa nchini Tanzania katika sekta ya kilimo, na nia yao ni kuona miradi hiyo inaleta matokeo chanya kwa wananchi.

Naye Prof. Najat Kassim Mohammed, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC), alieleza kuwa kulikuwa na mradi wa kilimo uliomalizika mwaka jana, na kikao kilichofanyika Zanzibar kitasaidia kufanikisha tafiti mpya zitakazosaidia kupambana na wadudu wanaoshambulia matunda, jambo litakalowaletea wananchi maendeleo ya moja kwa moja.

Ziara hiyo ilionyesha dhamira ya IAEA ya kuendeleza ushirikiano wake na Zanzibar, hususan katika sekta za kilimo na mifugo, ili kuongeza usalama wa chakula, kuboresha maisha ya wananchi, na kuimarisha maendeleo endelevu visiwani.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...