Na Seif Mangwangi, Michuzi TV, Arusha
Baraza Madiwani la Jiji la Arusha limejipanga kuwa Baraza la kwanza nchini kujiendesha kwa kutumia mapato ya ndani bila kutegemea ruzuku kutoka Serikali kuu.
Akifungua kikao cha pili cha robo mwaka cha Baraza la Madiwani wa Jiji hilo leo 13 Februari 2026, Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranghe amesema mpango wa Jiji hilo kujiendesha kwa mapato yake ya ndani pia umepitishwa na kuridhiwa kwenye vikao vya vya Madiwani wa Chama cha Mapinduzi ndani ya Baraza hilo.
Amesema kwa mwaka Jiji linauwezo wa kukusanya zaidi ya bilioni 150 Kwa mwaka huku Bajeti ya matumizi ikiwa ni bilioni 130 Kwa mwaka.
“ Kwa mapato ya Bilioni 150 bado tutakuwa na ziada ya bilioni 20 ambayo tutairudisha Serikalini ili iende kusaidia Halmashauri zingine za pembezoni, Kikubwa hapa tunatakiwa kukusanya mapato na kuboresha na kubuni vyanzo vipya vya mapato,” amesema.
Amesema mapato hayo yatapatikana kwa Jiji hilo kuboresha machinjio yake ya nyama iliyoko katika Kata ya sakina, kujenga hoteli za kitalii, kuboresha miundombinu ya barabara pamoja na stand Kwa kuingia ubia na watu binafsi kujenga jengo la biashara.
“Miaka 50 iliyopita Serikali ya china iliamua kuwekeza kwenye Serikali za mitaa katika miradi ya wananchi, ilikopa na hizo pesa inajenga miundo mbinu ya kutosha ndani ya mitaa, hivi sasa ni matajiri wakiwa,” amesema.
Aidha amewataka Madiwani kuwatangazia wananchi katika maeneo yao ya utawala kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na Jiji hilo huku akiagiza Idara ya Maendeleo ya Jamii kufuatilia marejesho kwa watu waliokopa.
Amesema fedha zinazotengwa kwaajili ya mikopo zimekuwa zikirudishwa na kupangiwa matumizi mengine baada ya kukosa watu wa kukopa jambo ambalo linarudisha nyuma kusudio la kutengwa Kwa fedha hizo.
Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt Maduhu Nindwa Kwa niaba ya Mkurugenzi John Kayombo amesema vurugu zilizotokea Oktoba 29, mwaka Jana 2025 baada ya uchaguzi mkuu zimesababisha uharibifu wa miundo mbinu ya zaidi ya bilioni 1.8.
Kutokana na uharibifu huo, Mkurugenzi ameliomba Baraza la Madiwani kuridhia kutumika kwa kiwango hicho cha fedha Ili kurejesha miundombinu hiyo ikiwemo Barabara pamoja na ukarabati wa majengo kwenye hali yake ya kawaida.
Akizungumza kwenye Baraza hilo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Joseph Mkude amewataka Madiwani kutumia hekima, utii na busara katika kuwatumikia wananchi Ili kuweza kuwaletea maendeleo.
Amesema kila mmoja akiwa na kiu ya kutatua matatizo ya wananchi watafanikiwa, “naomba Madiwani tuwe na upendo kwa wote, tufuate kanuni na taratibu, upendo, utii na nidhamu vinaenda pamoja, tukiwa tunaingia kazini tuzingatie haya yote,” amesema na kuongeza:
“Rais amekuwa akisisitiza suala la mapato na pia Meya amesisitiza wakati wa kufungua mkutano huu. Tuwe tuna hakikisha tunasimamia vyema suala la ukusanyaji wa mapato kwenye vyanzo vilivyopo,kuna vyanzo vingi vya mapato ambavyo hazikusanywi kufikia asilimia 100,” amesema.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...