Kwa masikitiko makubwa na huzuni nzito, tumepokea taarifa ya kifo cha Mwadhama Polycarp Cardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Marehemu alikuwa mchungaji mwaminifu na kiongozi mwenye hekima na busara, aliyeilitumikia Kanisa na Taifa kwa uaminifu mkubwa, akiacha alama isiyofutika katika mioyo ya wengi.

Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (TRAMEPRO), ninawasilisha salamu za rambirambi kwa Kanisa Katoliki, familia ya marehemu, waumini wote, na Watanzania wote walioguswa na msiba huu mkubwa katika Kanisa na Taifa letu.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, apumzike kwa amani ya milele.

“Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alikuwa kama sisi, nasi tutakuwa kama yeye; hivyo tujiandae.”

Imetolewa na:
Boniventura Mwalongo
Katibu Mkuu – TRAMEPRO

Tarehe: 24 Februari 2026





 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...