Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
MWANAFUNZI wa Uhandisi Tiba kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) wamekuja na ubunifu wa kifaa kinachoitwa BiliMeasure, kinachotumika kupima kiwango cha bilirubini inayosababisha homa ya manjano kwa watoto wachanga bila kuchukua sampuli ya damu.
Akizungumza katika Maonesho ya Pili ya Ubunifu ya MUHAS (Innovation Week 2026), yaliyofanyika leo Februaria 24, 2026 jijini Dar es Salaam mwanafunzi wa Uhandisi Tiba, Abubakar Mathias, alisema zaidi ya asilimia 60 ya watoto huzaliwa wakiwa na homa ya manjano, hali inayowalazimu kupelekwa kwenye kifaa maalumu cha tiba ya mwanga (phototherapy) kwa matibabu.
Alisema kifaa hicho kitafanya kazi sambamba na phototherapy kwa kupima maendeleo ya matibabu ya mtoto anayeugua manjano. Kifaa hicho huvalishwa mtoto kifuani au kichwani wakati wa matibabu na hupima kiwango cha bilirubini papo kwa papo bila maumivu.
“Kwa sasa vipimo vya manjano hutegemea sampuli ya damu, hali inayosababisha maumivu kwa watoto wachanga na usumbufu kwa wazazi pamoja na watoa huduma. Pia majibu ya maabara huchukua zaidi ya saa 12 hadi 24,” alisema.
Alieleza kuwa kifaa hicho kinatoa majibu ya muda halisi na hutoa taarifa kila baada ya dakika tano, hivyo kuondoa ucheleweshaji wa majibu ya maabara.
Mbali na kuondoa maumivu ya utoaji damu, kifaa hicho pia kinasaidia kudhibiti matumizi ya muda mrefu ya phototherapy (over treatment) ambayo inaweza kuleta madhara ikiwemo athari za mwanga kwa mtoto. Mtoto anapofikia kiwango stahiki cha bilirubini, kifaa hutoa alama ya sauti na mwanga kumuarifu mtoa huduma ili kuzima kifaa cha tiba ya mwanga.
Mathias alisema wamechukua mwaka mmoja kufanya utafiti, kuanzia hatua ya wazo, kufanya tafiti hospitalini na kwa watumishi wa afya, hadi kufikia hatua ya maendeleo ya kifaa hicho. Kwa sasa wanaendelea na maboresho ili kiweze kupitishwa na kutumika rasmi hospitalini, huku kilichobaki zaidi kikiwa ni uboreshaji wa muonekano wa nje (industrial design) na uchaguzi wa vifaa vya nje.

Mwanafunzi wa Uhandisi Tiba kutoka chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) mwenye fulana ya bluu akifafanua jambo kwa mtazamaji namna kifaa cha kupima homa ya manjano kwa watoto (billimeasure) kinavyofanya kazi wakati wa maonesho ya pili ya ubunifu ya MUHAS (Muhas innovation week 2026) leo Februari 24,2026

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...