IDARA ya Vijana ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Usharika wa Kanisa Kuu Iringa, kwa kushirikiana na huduma ya The Healing Missionaries kutoka Dar es Salaam, imeandaa mkesha mkubwa wa kusifu na kuabudu utakaofanyika Machi 20, 2026, mkoani Iringa.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Khery James, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tukio hilo la kiroho linalolenga kuwakutanisha waumini na wananchi kwa pamoja katika kumsifu na kumshukuru Mungu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Luckson maarufu kama Kaka Mtumishi, amesema lengo la mkesha huo ni kumsifu Mungu na kumshukuru kwa mambo makuu aliyoyatenda, huku akiwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki na kupokea baraka zitakazopatikana kupitia ibada hiyo.

Aidha, ameeleza kuwa mgeni mwenyeji atakuwa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Blaston Gaville, ambaye ataungana na viongozi wengine wa dini kuongoza ibada hiyo maalum.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa The Healing Missionaries, Patrick Mulunda, amesema taasisi hiyo imejikita katika kupeleka habari njema katika maeneo mbalimbali ambayo huduma haijafika, kwa lengo la kueneza Injili na kuwafikia watu wengi zaidi.

Mkesha huo unatarajiwa kupambwa na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili, sambamba na ushiriki wa viongozi wa dini na kijamii, katika tukio hilo maalum lenye lengo la kuimarisha imani, umoja na kumtukuza Mungu.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...