Na Diana Byera, Bukoba

WADAU wa brabara mkoani Kagera wamepata fursa ya kupokea taarifa  za mapendekezo ya bajeti kutoka kwa  Wakala wa Barabara Tanzania (TANROAD) pamoja na Wakala  wa Barabara za Mjini na Vijijini(TARURA).

Akizungumza mbele ya wadau hao Meneja wa TANROAD Mkoa wa Kagera Joel Samwel amesema TANROAD  wanakadiria kutumia Sh.bilioni 14.5 kwa mwaka wa fedha 2026/2027  kwa ajili ya  matengenezo ya barabara na madaraja.

Ameongeza kuwa ingawa bajeti halisi ya kusaidia matengenezo ya barabara madaraja  inayoweza kutosheleza vizuri Barabara za mkoa wa Kagera ni Sh.bilioni 25.8

Amesema Serikali imeendelea kutoa fedha za kukamilisha madaraja matano ya dharura ambayo yaliathiriwa na mvua kubwa za Elnino na sasa wananchi wataanza kutumia sehemu ya hizo kwa kipindi Cha mwaka mzima

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TARURA Mkoa wa Kagera Mahona Njigela amesema wakala huo unakadiriwa kutumia Sh.bilioni 23.7 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya matengenezo ya aina mbalimbali ya barabara , vivuko  na madaraja ili kusogeza huduma ya usafirishaji kwa wananchi.

Wakati huo huo kupitia  kikao hicho Mkuu wa Mkoa Mkoa wa Kagera Kanali  Yahya Ramadhan Kido amewaagiza TANROADS na TARURA mkoani humo kuzingatia na kutoa kipaumbele katika masuala ya ajira kwa vijana na wanawake wakati wa utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea  na inayotarajiwa kutekelezwa.

Pia amewataka TANROADS na TARURA kuzingatia usimamizi mathubuti wa raslimari fedha kwa maana asilimia ya kazi lazima ionekane thamani yake,ubora wa kazi kwa barabara zinazojengwa au kutengenezwa zidumu kuendana na matarajio na ushirikishwaji wa wananchi katika kulinda miundombinu ya barabara.

Kikao hicho kimeudhuriwa na wabunge wa Mkoa wa Kagera ambao wamesema wataongeza nguvu kwa serikali kwa ajili ya kuleta fedha ya barabara kwani mipango ya watendaji ni mizuri changamoto  ni fedha haziji kwa wakati katika miradi ya barabara.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...