Na WAF, Dar es Salaam

Wizara ya Afya kupitia Baraza la Tiba Asili imepeleka timu ya wataalam mkoani Dar es Salaam kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga  Mkuu wa Mkoa huo kwa lengo la kuwasajili waganga wa tiba asili.

Timu hiyo inaendesha zoezi la usajili kuanzia tarehe 09 hadi 20 Februari, 2026 katika Mtaa wa Mkunguni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mratibu wa zoezi hilo, Bi. Lucy Laurian, amesema lengo la usajili huo ni kuhakikisha waganga wote wa tiba asili wanafanya kazi kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na mamlaka husika.

“Tunawahimiza wataalam wote wa tiba asili kujitokeza kwa wingi kujisajili ili wapate vibali halali vya utoaji huduma. Kwa mujibu wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Sura ya 244 ya Sheria za Tanzania, ni kosa kwa mtu yeyote kutoa huduma za tiba asili bila kusajiliwa na Baraza,” amesema Bi. Laurian.

Ameongeza kuwa kifungu cha sheria hiyo kinampa mamlaka Msajili na Baraza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya yeyote anayekiuka masharti ya usajili, ikiwemo kutozwa faini au kuchukuliwa hatua nyingine kwa mujibu wa sheria.

Wizara ya Afya imesisitiza kuwa zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuboresha na kurasimisha huduma za tiba asili nchini, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma salama, zenye viwango na zinazotambuliwa kisheria.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...