Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari amesema Serikali imeongeza msukumo wa mageuzi ya sheria za usafiri wa anga nchini.
Akifungua Warsha juu ya Mikataba ya Sheria za Anga ya mwaka 2026 iliyoandaliwa na TCAA kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO), Mheshimiwa Johari alisema sekta ya anga inakabiliwa na mageuzi makubwa yanayotokana na matumizi ya Akili Bandia (AI), ndege zisizo na rubani, mifumo ya kidijitali na ongezeko la vitisho vya usalama mtandao.
Mhe. Johari, aliongeza kuwa, kwa kutoa wito wa kuharakishwa kwa uridhiaji na uingizaji wa mikataba ya kimataifa ya anga katika sheria za kitaifa ili kuendana na mabadiliko ya kasi katika sekta hiyo.
Alibainisha kuwa ingawa teknolojia hizi zinafungua fursa kubwa za ubunifu na ufanisi, pia zinaibua maswali magumu ya kisheria na kimaadili. Hivyo, alisisitiza umuhimu wa nchi kutafakari upya namna ya kutunga, kusimamia na kutekeleza sheria za anga.
Mheshimiwa Johari alieleza kuwa usafiri wa anga una mchango mkubwa katika kuunganisha watu, masoko na tamaduni, kuchochea ukuaji wa uchumi, biashara na utalii. Hata hivyo, alionya kuwa manufaa hayo yanategemea mfumo thabiti na ulioratibiwa wa sheria za kimataifa za anga.
Warsha hiyo ya siku tatu imewakutanisha zaidi ya washiriki 150, wakiwemo takriban wajumbe 70 kutoka mataifa mbalimbali, kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu mikataba ya anga, kubainisha faida na wajibu wa nchi wanachama, na kujadili mbinu za uridhiaji na utekelezaji wake.
Na kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Bw. Salim Msangi, alisema warsha hiyo ni jukwaa muhimu la kujifunza na pia kichocheo cha mageuzi ya ndani. Alieleza kuwa TCAA inatumia fursa hiyo kutathmini mikataba ambayo Tanzania haijaridhia na kuharakisha hatua za kuiingiza katika sheria za kitaifa.
Alifafanua kuwa kuridhia mikataba ya kimataifa kunasaidia kuleta uwiano wa taratibu na hatua za kiutendaji miongoni mwa nchi wanachama, hivyo kuongeza uhakika na utabirika katika shughuli za usafiri wa anga wa kimataifa.
Naye, Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Mahusiano ya Nje wa ICAO, Bw. Michael Gill, alisisitiza kuwa uridhiaji na utekelezaji wa mikataba ya kimataifa ya anga ni msingi wa kuhakikisha usafiri wa anga ulio salama, wa uhakika na endelevu duniani. Alibainisha kuwa tangu mwaka 1947, Kamati ya Sheria ya ICAO imeandaa mikataba 24 inayounda msingi wa mfumo wa kisheria wa usafiri wa anga duniani chini ya Mkataba wa Chicago, uliotimiza miaka 80 hivi karibuni.
Aliongeza kuwa Mpango Mkakati mpya wa ICAO wa 2026–2050 unaweka msisitizo zaidi katika kuimarisha uwezo wa kisheria wa nchi wanachama na kuoanisha sheria za anga ili kukabiliana na changamoto mpya za kimataifa.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Hamza Johari akizungumza wakati wa hotuba yake ya ufunguzi wa Warsha juu ya Mikataba ya Sheria za Anga ya mwaka 2026 iliyoandaliwa na TCAA kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Salim Msangi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha juu ya Mikataba ya Sheria za Anga ya mwaka 2026 iliyoandaliwa na TCAA kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO)
Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria na Mahusiano ya Nje wa ICAO, Bw. Michael Gill akitoa salam kwa niaba ya ICAO wakati wa ufunguzi wa Warsha juu ya Mikataba ya Sheria za Anga ya mwaka 2026 iliyoandaliwa na TCAA kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO)
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria TCAA Bi. Maria Memba wakati wa ufunguzi wa Warsha juu ya Mikataba ya Sheria za Anga ya mwaka 2026 iliyoandaliwa na TCAA kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO)
Washiriki wakisikilza yanayojiri wakati wa ufunguzi wa Warsha juu ya Mikataba ya Sheria za Anga ya mwaka 2026 iliyoandaliwa na TCAA kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani (ICAO)
Picha za pamoja





















Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...