Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauniakizungumza wakati akifungua Semina kwa Wajumbe wa Baraza la WawakilishiZanzibar kuhusu Elimu ya Muungano iliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano waBaraza la Wawakilishi Unguja, Zanzibar, Februari 27, 2026.


MWANDISHI WETU, UNGUJA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Hamad Yussuf Masauni, amewaasa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kuelimisha wananchi kuhusu misingi, faida nawajibu wao katika kulinda na kuutetea Muungano,

Pia amewataka Kupinga na kusahihisha upotoshaji wa taarifa kuhusu Muungano, hususanikupitia mikutano ya hadhara na mitandao ya kijamii.

Amesema, kwa kufanya hivyo, Wawakilishi watakuwa mabalozi wa amani, umoja namshikamano wa kitaifa, kusikiliza na kuwasilisha.

Waziri Masauni aliyasema hayo Februari 27,2026 wakati akifungua semina ya elimu yaMuungano kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, ikiwa ni sehemu ya mpango unaoendeleawa kutoa elimu hiyo kwa makundi mbalimbali ya jamii.

Amesema, kwa ujumla Wawakilishi ni nguzo muhimu ya kulinda na kuimarisha Muungano waTanzania kwa kupitia kutunga sheria, kusimamia Serikali na kuelimisha wananchi.

“Wawakilishi mnabeba dhamana ya kihistoria ya kuhakikisha Muungano unaendelea kuwachanzo cha amani, mshikamano wa pande mbili na maendeleo,” alisema

Amesema, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni nguzo muhimu katika kuendelea kuuelimishana kuulinda Muungano wa Tanzania kwa kuwa wako karibu zaidi na wananchi.

Amesema, Wajumbe hao wana nafasi kubwa ya kuifikisha elimu ya Muungano kwa wananchi kwa sababu wanawakilisha na kukutana na wananchi mara kwa mara katika majimbo yao.

“Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni nguzo muhimu katika kuulinda Muungano wetu, wanawafikia wananchi wengi zaidi, hivyo wana wajibu wa kueneza elimu ya Muungano katikamaeneo yao,” amesema

Ameeleza kuwa kwa kiasi kikubwa mpango huo unawalenga vijana ili waweze kufahamu fursazilizopo ndani ya Muungano na kuzitumia kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Amesema, fursa za Muungano ni nyingi, lakini changamoto iliyopo ni kutokuzitangaza nakuzifafanua ipasavyo kwa wananchi.

Kupitia semina hiyo mada mbali mbali zimewasilishwa kama vile Chimbuko, Misingi, Umuhimu wa Muungano, na Upekee wa Muungano.

Amesema, kupitia mada hizo wawakilishi hao watakuza na kuongeza uelewa na kutoa taswirapana juu ya umuhimu wa uwepo wa Muungano na kuibua hamasa ya katika kujenga uzalendowa dhati kwa nchi, kuudumisha na kuuenzi Muungano kwa manufaa ya kizazi cha sasa nakijacho.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Richard Muyungi, amesema ofisi hiyo itaendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ilikuhakikisha uelewa wa masuala ya Muungano unaongezeka na kuimarika.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauniakizungumza wakati akifungua Semina kwa Wajumbe wa Baraza la WawakilishiZanzibar kuhusu Elimu ya Muungano iliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano waBaraza la Wawakilishi Unguja, Zanzibar, Februari 27, 2026.
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika semina kuhusuMuungano iliyofanyika katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Unguja, Zanzibar, Februari 27, 2026.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Richard Muyungi (kushoto) akiwa miongonimwa viongozi walioshiriki semina kuhusu elimu ya Muungano iliyotolewa kwa Wajumbewa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi Unguja, Zanzibar, Februari 27, 2026.

PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...