Mhe. Daniel G. Chongolo (Mb.), Waziri wa Kilimo amefanya kikao na Bw. Ernest Ruzindaza, Mratibu Msimamizi wa Programu ya Mifumo Himilivu ya Chakula (TFSRP) na Mchumi Mkuu kutoka Benki ya Dunia ambayo ni programu iliyo chini ya Wizara ya Kilimo.
Kikao hicho kimefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Afrika kuhusu Matumizi Endelevu ya Zana za Kilimo (Africa Conference on Sustainable Agricultural Mechanization – ACSAM) unaofanyika kuanzia tarehe 3-6 Februari 2026.
Pamoja na mambo mengine, wamezungumza kuhusu ukaguzi wa utekelezaji (medium term review) wa Programu ya TFSRP baada ya Programu hiyo kufikisha nusu ya muda wake tangu ianze miaka na nusu iliyopita.
Bw. Ruzindaza ameeleza kuwa matokeo ya ukaguzi huo yataonesha maeneo ambayo yatahitaji kuongeza nguvu zaidi; huku pia kuonesha maeneo yanayohitaji kupunguza vipaumbele.
Aidha, Mheshimiwa Waziri amejadiliana pia na Bw. Ruzindaza kuhusu wafadhili wengine waliojitokezo kuonesha nia ya kufadhili programu hiyo ambao ni pamoja na IFAD, JICA na Agri Connect.
Wengine walioshiriki katika kikao hicho ni Bw. Gerald Mweli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo na Bw. Timotheo Semuguruka, Mratibu wa programu ya TFSRP katika Wizara ya Kilimo.


.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...