Na Josephine Majura na Peter Haule, WF, Dar es Salaam



Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza Mhe. Marianne Young pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Waziri alisisitiza dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuimarisha sekta mbalimbali, hususan zile zinazogusa moja kwa moja maisha ya wananchi.

Alibainisha kuwa ushirikiano wa nchi na nchi ni chachu ya kufanikisha miradi ya maendeleo na kuongeza ustawi wa kijamii na kiuchumi.

Aidha, Mhe. Balozi Omar, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kufanya shughuli zake kwa uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku akiwahakikishia washirika wa maendeleo kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana kwa dhati ili kufanikisha malengo ya pamoja.

Kwa upande wao, Mabalozi wa Uingereza na Sweden walieleza kuwa nchi zao zinathamini uhusiano wa muda mrefu na Tanzania na wataendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Melckzedeck Mbise na Wajumbe kutoka Ubalozi wa Uingereza na Sweden.

Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiagana na Balozi wa Sweden nchini, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, baada ya mkutano kati yao kuhusu ushirikiano wa Maendeleo, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiteta jambo na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias, baada ya mkutano kati yao kuhusu ushirikiano wa maendeleo, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akisikiliza maelezo ya Balozi wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias, kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Sweden, kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (wa nne kushoto), akiongoza mkutano kati yake na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias, (hayupo pichani), kuhusu ushirikiano wa maendeleo, uliofanyika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.

 

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...