Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Daud Yassin amesema siku 100 tangu kuingia madarakani kwa Rais, Dkt Samia zimekuwa na mwanga mkubwa wa kuleta maendeleo nchini.

Amesema kazi nyingi zimeendelea kutekelezwa huku changamoto za Watanzania zikitatuliwa kupitia sekta zote.

Akizungumza katika taarifa yake kupitia mitandao ya kijamii, Yassin amesema amani na utulivu vimeifanya Tanzania kuendelea kung'aa zaidi.

"Siku 100 za Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan zimekuwa zenye mwanga mkubwa wa maendeleo katika nchi yetu," amesema Yassin.

Yassin amesema anaungana na Watanzania wote kumtakia heri Dkt Samia na viongozi wote katika utekelezaji wa majumu yao.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...