Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imefanya ziara ya kikazi mkoani Geita kukagua miradi inayosimamiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ambapo imemwagiwa sifa kwa mapinduzi ya teknolojia kwa wachimbaji wadogo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo katika eneo la Katente, Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa, ameeleza kuwa serikali kupitia STAMICO imejikita kuhakikisha wachimbaji wadogo wanajifunza kwa nadharia na vitendo.
Dkt. Kiruswa amebainisha kuwa kituo hicho kinahudumia zaidi ya wachimbaji wadogo 1,019, ambao sasa wana uwezo wa kuleta marudio yao (mbare) na kuondoka na dhahabu iliyo safi ndani ya muda mfupi kutokana na matumizi ya teknolojia ya kisasa ya CIP.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgalu, ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha vituo vya mfano vinavyowasogezea wataalam karibu na wachimbaji.
"Ni wakati sasa kwa STAMICO na Wizara ya Madini kuona namna ya kuongeza ukubwa wa vituo hivi ili kutoa huduma kwa wachimbaji wengi zaidi na kwa uharaka zaidi," alisisitiza Mhe. Mgalu.
Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO, Bw. Deusdedith Magala, ametoa shukrani kwa Kamati hiyo kwa kuridhishwa na uwekezaji wa shirika hilo. Amesema jitihada hizo zinalenga kuhakikisha huduma za serikali zinafika moja kwa moja kwa walengwa katika sekta ya madini.


.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...