Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa (kushoto), akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, alipofika kumtembelea akiwa na ujumbe wake, ofisini kwake, mjini Mbeya jana. Bw. Laiser na ujumbe wake wapo mjini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Mwilongo Msungu, wakati Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser (Katikati), na ujumbe wake, ukimtembela mkuu wa mkoa huyo, ofisini kwake, mjini Mbeya jana. Bw. Laiser na ujumbe huo wapo mjini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa (kushoto), akiwa na baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania, wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser (hayupo pichani), na ujumbe wake, walipomtembelea mkuu wa mkoa huyo, ofisini kwake, mjini Mbeya jana. Bw. Laiser na ujumbe huo wapo mjini Mbeya kwa ziara ya kibiashara. Katikati ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere na Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi, Bi. Mwilongo Msungu.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa (kulia), akiagana na Mkuu wa Mikakati na Data wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. John Mosha, wakati yeye, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo, walipomtembelea mkuu  wa mkoa huyo, ofisini kwake, mjini Mbeya jana. Bw. Laiser na ujumbe huo wapo mjini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa (kulia), akiagana na Meneja wa Benki ya Absa mkoani humo, Bw. Alto Hagamu, na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Melvin Saprapasen (kushoto), wakati wao, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser (hayupo pichani), pamoja na maofisa wengine wa benki hiyo, walipomtembelea mkuu  wa mkoa huyo, ofisini kwake, mjini Mbeya jana. Bw. Laiser na ujumbe huo wapo mjini Mbeya kwa ziara ya kikazi.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Beno Malisa (wa sita kushoto), akipozi kwa picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kulia kwake), mara baada ya  mkurugenzi huyo pamoja na ujumbe wake kumtembelea ofisini kwake mjini Mbeya jana wakiwa mkoani humo kwa ziara ya kikazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...