Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetangaza azma ya kuanzisha chombo maalum kitakachosimamia rasilimali za uvuvi, lengo likiwa ni kulinda mazao yanayotokana na Ziwa Victoria dhidi ya uharibifu.
Hatua hii imekuja baada ya wataalamu wa wizara hiyo waliopelekwa wilayani Chato kutoa elimu kwa vitendo, kubaini kuwepo kwa wimbi kubwa la uvuvi haramu katika eneo hilo.
Katika operesheni hiyo iliyofanywa na wataalamu hao wakati wakitekeleza majukumu yao, mafanikio makubwa yamepatikana ambapo zana zifuatazo zimekamatwa Nyavu haramu 60,Injini za boti 40,Boti 60 na Matanki matatu (3) ya mafuta.
Akizungumza wakati wa ziara yake wilayani Chato, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Bashiru Ally, amebainisha kuwa Mamlaka ya Usimamizi wa Mazao ya Ziwa imeundiwa kanuni kali. Moja ya kanuni hizo ni kupiga marufuku uvuvi wa samaki wachanga walio chini ya sentimita 10, hatua inayolenga kulinda kizazi cha samaki ndani ya Ziwa Victoria.
Waziri Bashiru ametoa wito kwa viongozi wa wilaya ya Chato kuacha mara moja tabia ya kuwatetea wavuvi haramu. Amewataka kusimamia Ilani ya Chama inayoelekeza ulinzi wa rasilimali za nchi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Ulinzi wa Rasilimali za Uvuvi, Furaha Bulonga, amefichua changamoto iliyobainika wakati wa utoaji elimu:
"Tumebaini elimu haiwafikii wamiliki wa vyombo moja kwa moja, badala yake inawafikia wafanyakazi tu ambao hupokea maelekezo kutoka juu," alisema Bulonga.
Katika hatua nyingine, Waziri Bashiru ametoa siku saba (7) kwa mkandarasi pamoja na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kukamilisha mradi wa Mwalo wa Chato Beach.
Agizo hilo limekuja baada ya Waziri kukagua majengo ya soko hilo na kubaini kasoro kadhaa, hali iliyompelekea kugoma kupokea mradi huo mpaka marekebisho yafanyike ili uanze kufanya kazi kwa ufanisi.



.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...