Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma 

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Wanu Hafidh Ameir amesema kuwa Serikali imezidi kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Kidijitali kama nyenzo muhimu katika kuongeza ufanisi wa utoaji Elimu,dhamira ikiwa ni kuwa kichocheo cha ubunifu na kuzalisha maarifa kwa Wanafunzi.

Ambapo amesema ili kufanikisha hilo Serikali imeandaa na kuanza kutekeleza mkakati wa Kitaifa wa matumizi ya Teknolojia ya Kidijitali katika Elimu pamoja na miongozo yake ikiwemo muongozo wa matumizi ya Tehama katika Shule na Vyuo vya Ualimu na muongozo wa akili unde katika Elimu hiyo.

Mhe Naibu Waziri huyo ameyasema hayo mapema leo hii Jijini Dodoma Machi 30,2026 katika hafla ya ugawaji vifaa vya Tehama kwaajili ya kufundishia na kujifunzia katika Shule za Msingi na Sekondari Nchini.

"Serikali ya awamu ya sita inaendelea kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Kidijitali kama nyenzo muhimu ya kuongeza ufanisi wa utoaji wa Elimu,dhamira ikiwa ni kuhakikisha kuwa Teknolojia haitumiki tu kama chombo cha kujifunzia bali pia inakuwa kichocheo cha ubunifu na uzalishaji wa maarifa kwa vijana wetu".

Aidha katika zoezi hilo la ugawaji wa vifaa vya Tehama Naibu Waziri Wanu ametoa wito kwa Walimu,Wanafunzi na Wadau wa Elimu kwa ujumla kutumia na kuvitunza vifaa hivyo ipasavyo ili viweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa kama ambavyo inaelekezwa katika Sera ya Elimu na katika Dira ya Maendeleo ya 2050,Serikali imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kuboresha Elimu kwa kuzingatia mahitaji ya karne ya 21 ikiwemo kuimarisha matumizi Teknolojia za Kidijitali katika ufundushaji na ujifunzaji.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi Lyra in Afrika ambayo imeshirikiana na Serikali katika upatikanaji wa vifaa hivyo Mhandisi Kulaya Henry ameeleza kuwa Shirika hilo limekuwa likishirikiana na Serikali na hata jamii katika mambo mbalimbali ikwemo ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule za Sekondari za Kata za Vijijini kwa Mkoa wa Iringa na Dodoma ambapo mpaka sasa wamejenga mabweni 16 katika shule 11 kwa Wilaya 3 za Mkoa wa Iringa na 1 kwa Wilaya ya Chamwino Dodoma.

Akitoa neno la Shukurani kwa niaba ya Wakuu wa Shule 9 zilizopoke vifaa vya Tehama Mwalimu Ignus Komba kutoka Shule ya Sekondari ya amali Iyunga amesema vifaa hivyo vinakwenda kuongeza umahiri na ufaulu mkubwa kwa wanafunzia,pamoja na kuahidi kwenda kusimamia matumizi sahihi na bora ya vifaa hivyo ili wanafunzi waweze kupata umahiri na kupandisha ufaulu wa Shule zao.

Leo vimetolewa jumla ya vifaa 1510 vikiwemo uhalisia pepe na simu janja ambavyo vimegawanyika katika makundi 15 vikiwa vimegharimu Shilingi Milioni 769 na laki 390 na vitakwenda katika Shule za msingi na Sekondari katika Mikoa 9 kwa Tanzania Bara na Visiwani ikiwemo Kusini Unguja,Dodoma,Mtwara, Geita na Arusha.




 

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...