Na Mwandishi wetu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Mwenda, amezitaka kampuni za Kichina na wafanyabiashara wote nchini kuzingatia kikamilifu sheria za kodi kwa kulipa kwa wakati, kutoa taarifa sahihi, na kushirikiana kwa karibu na mamlaka hiyo.
Akizungumza katika Mkutano wa Mafunzo na Kubadilishana Uzoefu wa Kodi kati ya Biashara za Tanzania na China 2026 uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenda alisema kuwa ni wajibu wa kila kampuni—iwe ya binafsi au ya Serikali—kufuata taratibu za kodi kwa uaminifu, ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya kidijitali katika usajili na ulipaji wa kodi.
Alisisitiza umuhimu wa uwazi na usawa katika utekelezaji wa majukumu ya kikodi, akibainisha kuwa uratibu mzuri kati ya TRA na walipa kodi utasaidia kuepusha migongano isiyo ya lazima.
“Tunathamini mchango wa wawekezaji katika maendeleo ya taifa na tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi kwa uwazi na ushirikiano endelevu,” alisema Mwenda.
Kwa upande wake, Balozi wa China nchini Tanzania, Bi. Chen Mingjian, alizitaka kampuni za Kichina zinazofanya biashara nchini kuzingatia kikamilifu sheria na kanuni za kodi za Tanzania, kulipa kodi stahiki, na kuepuka vitendo vya ukwepaji kodi.
Alisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya kampuni hizo na TRA ili kuhakikisha uwazi na ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
Aidha, Balozi Chen alieleza kuwa matumizi ya mifumo ya kisasa ya TEHAMA yanawezesha kampuni kupata taarifa sahihi na za wakati kuhusu masuala ya kodi, hatua inayosaidia kupunguza changamoto zilizokuwepo hapo awali.
Aliongeza kuwa juhudi hizo zinaendana na azma ya Serikali ya Tanzania ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara, akirejea pia mpango wa maboresho ya mfumo wa kodi uliotangazwa hivi karibuni unaojumuisha mapendekezo 284, wenye lengo la kuufanya mfumo huo kuwa wa kisasa zaidi, rafiki kwa walipa kodi, na wenye ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...