Shirika lisilo la kiserikali la Kikristo ECHO East Africa kutoka Ngaramtoni jijini Arusha limefanya warsha ya mafunzo kwa vitendo kwa waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha kuhusu Kilimo Ikolojia (Agroecology).
Shirika hilo linafanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika, Lengo ni kuwasaidia wakulima, hususan wakulima wadogo, kwa kuwapatia mbinu mbadala, elimu, ujuzi na maarifa ili kuongeza uzalishaji wa mazao yao kwa kutumia mbinu rafiki kwa mazingira, ikiwemo kilimo ikolojia.
Warsha hiyo ya mafunzo kwa vitendo imefanyika kwa siku mbili na Dhumuni la mafunzo hayo ni kuwaleta pamoja waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali ili kuwafahamisha juu ya uwepo wa shirika hilo, kuelewa shughuli mbalimbali zinazotekelezwa, pamoja na kuwapa elimu kuhusu kilimo ikolojia.
Katika mafunzo hayo, waandishi wa habari wamepata fursa ya kufanya ziara katika maeneo mbalimbali ndani ya shirika hilo na kujifunza masuala kadhaa ya kilimo ikolojia. Miongoni mwa mambo waliyojifunza ni pamoja na mbinu za uvunaji wa maji ili kupunguza mmomonyoko wa udongo, kilimo mseto, upandaji wa miti, na matumizi ya mazao yanayofunika ardhi ili kulinda rutuba ya udongo.
Aidha, washiriki wametembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo, ikiwemo benki ya mbegu, uzalishaji wa biogas, matumizi ya mitambo ya kukaushia vyakula, pamoja na kutembelea wakulima ambao ni wanufaika wa mbinu za kilimo ikolojia.
Kilimo Ikolojia (Agroecology) ni mfumo wa kilimo unaochanganya kanuni za ikolojia, yaani mazingira ya asili, na uzalishaji wa mazao. Lengo lake ni kuzalisha chakula kwa njia rafiki kwa mazingira, endelevu na yenye kunufaisha wakulima pamoja na jamii kwa muda mrefu.
Wataalamu wa kilimo wanaendelea kuhamasisha matumizi ya kilimo ikolojia kama njia mbadala ya kuongeza uzalishaji wa chakula huku wakilinda mazingira. Mbinu hii inahusisha matumizi ya rasilimali za asili, kupanda mazao mchanganyiko, pamoja na kupunguza utegemezi wa kemikali shambani.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...