Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, ameiomba Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kusimamia kikamilifu utoaji wa hati za ardhi ili kuhakikisha zinazingatia taratibu na mipango miji, akisema kuwa uzembe katika mchakato huo unachangia kuongezeka kwa migogoro ya ardhi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa programu ya Samia Ardhi Kliniki, Mpogolo alisema baadhi ya hati zimekuwa zikitolewa bila kuzingatia ramani na mpangilio rasmi wa maeneo, hali inayosababisha wananchi kujenga katika maeneo yasiyoruhusiwa ikiwemo kuziba barabara.

“Tusipofuata taratibu za upangaji miji, tutazalisha migogoro mikubwa katika jamii. Watu wanajikuta wanaziba barabara au kujenga katika hifadhi za wazi kwa sababu ya makosa ya kiutendaji,” alisema Mpogolo.

Aidha, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Samia Ardhi Kliniki ili kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Ardhi, ikiwemo ushauri wa kitaalamu, uhakiki wa nyaraka, pamoja na utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Katika hatua nyingine, Mpogolo ameipongeza Wizara ya Ardhi kwa kuanzisha kliniki hiyo, akieleza kuwa itasaidia kupunguza malalamiko ya muda mrefu na kuimarisha uwazi pamoja na uwajibikaji katika sekta ya ardhi.

Aliongeza kuwa ushirikiano kati ya serikali na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha mipango miji inaheshimiwa na maendeleo yanafanyika kwa utaratibu unaokubalika kisheria.
Naibu Katibu Mkuu Bi. Lucy Kabyemera akimkabidhi hati Miliki ya Ardhi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Edrward Mpogolo katika tukio la uzinduzi wa Samia Ardhi Kliniki jijini Dar es Salaam tarehe 2 Machi 2026. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Milki Wizara ya Ardhi Dkt Upendo Matotola

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...