WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amewasili mkoani Kigoma hii leo, Alhamisi Aprili 16, 2026, ambako anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Ziwa Tanganyika (Lake Tanganyika Business and Investment Forum).
Kongamano hilo linawakutanisha viongozi wa Serikali, wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika, zikiwemo Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Tanzania ambayo ni mwenyeji wa kongamano hilo lililoanza jana Jumatano, Aprili 15 ambapo litatamatika Jumamosi, Aprili 18, 2026.
Akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Simon Sirro.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...