Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Dk Juma zuberi Homera Aprili 11, 2026, Amekabidhi rasmi magari mawili kwa Ofisi ya TANESCO wilayani Namtumbo, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kasi ya utoaji wa huduma ya umeme katika jimbo letu.

Kupatikana kwa magari haya ni sehemu ya juhudi endelevu za kuboresha miundombinu na kuimarisha upatikanaji wa huduma muhimu kwa wananchi, hususan katika maeneo ya vijijini na pembezoni.

Magari hayo yanatarajiwa kurahisisha shughuli za kiutendaji, ikiwemo usimamizi wa miradi ya umeme, matengenezo ya miundombinu, pamoja na kushughulikia changamoto za huduma kwa wakati.

Aidha Mh Mbunge Amepongeza TANESCO kwa jitihada zake madhubuti katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme kwa uhakika, hatua ambayo inaendelea kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika maeneo mbalimbali.

"Ninawapongeza watumishi wa taasisi hiyo kwa kujituma kwao na kuwasihi kuyatunza vyema magari hayo ili yaweze kudumu na kutoa tija iliyokusudiwa. Matumizi sahihi ya rasilimali hizi ni muhimu katika kufanikisha azma ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi".









Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...