MSIMU wa mbio za Mac D Promotions ‘ Mac D Marathon’ kwa mwaka 2026 unatarajiwa kufanyika Julai 4 mwaka huu katika viwanja vya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC,) Kwa kauli mbiu ya ‘Go Green With Gas’ yenye kulenga kuhamasisha matumizi ya nishati safi na kutunza misitu.
Akizungumza katika uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mipango na Biashara wa Mac D Promotions Denzel Rweyunga amesema kuwa mbio hizo ambazo usajili wake umeanza rasmi leo zinatarajiwa kushirikisha wakimbiaji wa Kilomita 5, 10 na 21 pamoja na mbio za watoto za Kilomita 2.
Amesema kuwa licha ya kuhamasisha utunzaji wa afya kwa kukimbia mbio hizo pia zimelenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutunza mazingira kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi.
“Tunategemea kuwa na washiriki 3500 katika mbio hizi na maandalizi yameanza mapema ili kuzipa hadhi na viwango vya juu, na tayari usajili umefunguliwa kupitia www.macdmarathon.com na baada ya kujisajili na kufanya malipo kupitia simu au benki washiriki wataweza kupata vifaa zikiwemo tisheti katika vituo mbalimbali vilivyoainishwa.” Amesema.




.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...