MAHAKAMA Kuu Masijala Ndogo Dar es salaam, imetupilia mbali maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kuomba kuunganishwa katika kesi ya mgawanyo wa mali iliyofunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Said Issa Mohamed, pamoja na wenzake.
Wengine waliofungua kesi hiyo hiyo ni wajumbe wa bodi ya wadhamini wa Zanzibar Ahmed Rashid Khamis na Maulidah Anna Komu (marehemu).
Wajibu maombi katika kesi hiyo namba 8323 ya mwaka 2025 ambao ni Bodi ya Wadhamini ya Chadema upande wa bara na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika.
Uamuzi huo mdogo umetolewa na Jaji Hamidu mwanga ambaye awali alikuwa akikisikikiza shauri hilo na umesomwa leo Aprili 30, 2026 na Naibu Msajili ya Mahakama hiyo, Hussein Mushi.
Awali, kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa mbele ya Jaji Mwanga kama ilivyoelezwa, huku Lissu aliomba kuunganishwa katika kesi hiyo akidai kuwa kwakuwa kesi hiyo inahusu chama na yeye ndiye mwenyekiti wa chama basi anapaswa kuwa sehemu ya kesi hiyo.
Maombi hayo yalisikilizwa na uamuzi ulipaswa kutolewa Machi 25, mwaka huu lakini kutokana na faili kuitwa Mahakama ya Rufaa Dodoma kesi hiyo ilipelekwa mbele hadi leo.
Katika uamuzi huo Mahakama imekataa kumuunganisha Lissu katika kesi hiyo kama mwenyekiti wa Chama lakini kwakuwa ameyapeleka kwa matakwa yake na si kwa nafasi yake hivyo hana maslahi ya moja kwa moja kwani cheo hicho kinaweza kukaliwa na mtu yeyote
Mahakama imeeleza kuwa Lissu anaweza kutokea kwenye kesi hiyo kama shahidi wakati wa usikilizwaji wa kesi ya msingi na si kama moja ya wajibu maombi
Akizungumza nje ya Mahakama Wakili wa chadema , Dkt. Rugemeleza Nshala amedai kesi hiyo kwa sasa imehamishiwa kwa Jaji David Ngunyale na inatarajiwa kutajwa Mei 13,2026.
"Kurudi kwa kesi hii kunaenda sambamba na kufuata maagizo ya mahakama ya Rufaa ya kumtaka Jaji huyo kuangalia kama maombi hayo yalipelekwa ndani ya muda au laa.
“Madai yanatakiwa yaletwe ndani ya miaka sita tangu kuanza kwa migogoro katika uamuzi wa leo wa Jaji Mwanga wakili wa upande wa walalamikaji alisema kwa msisitizo kwamba mgogoro ulianza mwaka 2016, hivyo jaji Ngunyale atatusaidia kuangalia ni muda gani kati ya 2016 hadi 2025,” ameeleza Dkt. Nshala.
Akizungumzia kesi ya uhaini dhidi ya Lissu, Dkt Nshala bado hawajajua itapangwa lini kwa sababu kesi hiyo ipo katika Mahakama ya rufaa ambayo ndo inatarajiwa ipange mara nyingi hupangwa kwa muundo wa vikao, hivyo msajili wa Mahakama ya rufaa ndiyo atajua ipangwe lini,” amedai Dkt Nshala.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...