Na Janeth Raphael-MichuziTv
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesisitiza dhamira ya serikali kuendelea kuimarisha mazingira ya kazi na ustawi wa kundi la Mama na Baba Lishe nchini, akibainisha kuwa serikali inaendelea kutambua mchango wao muhimu katika uchumi wa taifa.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Kongamano la Kitaifa la Mama na Baba Lishe, Rais Samia alisema serikali imekuwa ikifuatilia changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao wadogo na imeweka mikakati mahsusi ya kuzitatua hatua kwa hatua.
“Changamoto zenu (Mama na Baba Lishe) tunazifahamu na si ngeni kwetu. Serikali inaendelea kuzifanyia kazi, na tuna mikakati mahususi ya kuendeleza kundi hili muhimu,” alisema Rais Samia.
Kuhusu ombi la kuwa mlezi wa kundi hilo, Rais Samia alieleza kuwa akiwa kiongozi wa nchi tayari ni mlezi wa makundi yote, lakini aliahidi kutoa kipaumbele maalum kwa Mama na Baba Lishe baada ya kumaliza majukumu yake ya urais, endapo atakuwa hai.
“Nikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nakuwa mlezi wa makundi yote ndani ya nchi. Hata hivyo, kwa kundi hili nitatoa kipaumbele kwamba baada ya kumaliza kazi ya Urais na nikiwa hai in shaa Allah nitakuwa mlezi wa kundi hili,” alisema.
Aidha, Rais aligusia suala la huduma za ulezi wa watoto, akibainisha kuwa serikali itaendelea kuboresha miundombinu itakayowezesha wazazi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi bila kubeba watoto wakati wa shughuli zao.
“Kuna haja ya kuwa na vituo vya ulezi wa watoto. Hii ni haki ya watoto na pia itawasaidia mama zao kufanya kazi bila kuwabeba migongoni, jambo ambalo linaweza kuathiri afya zao,” alieleza.
Katika hatua nyingine, Rais Samia alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mikopo na huduma mbalimbali za kifedha ili kuwawezesha kupata mitaji na kukuza biashara zao.
Akizungumzia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Rais alisema utekelezaji wake utazingatia ushirikiano wa sekta mbalimbali, ambapo sekta binafsi itakuwa na mchango mkubwa zaidi.
“Maendeleo yetu yatatekelezwa kwa aina tatu; Serikali asilimia 22, sekta binafsi asilimia 70, na mashirika ya umma asilimia 8. Hivyo ni lazima tufanye kazi kwa karibu na sekta binafsi,” alisema.
Kongamano hilo limewakutanisha Mama na Baba Lishe kutoka maeneo mbalimbali nchini, likilenga kujadili changamoto zao na kuweka mikakati ya kuboresha mazingira ya biashara zao.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...