Babati, Manyara
Halmashauri ya Mji wa Babati mkoani Manyara ni miongoni mwa miji inayonufaika na utekelezaji wa mradi wa Uendelezaji wa Miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) stendi mpya ya kisasa, barabara za lami pamoja na miradi mingine ya kijamii itajengwa kupitia mradi huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, CPA. Shaaban Mpendu alibainisha hayo nakueleza kuwa wamepokea zaidi ya shilingi Bilioni 20.5 kwa ajili ya kujenga Stendi mpya ya kisasa ya mabasi itakayokuwa Stendi ya mkoa wa Manyara, barabara za katikati ya mji pamoja na mitaro ya maji ya mvua na maji taka kupitia mradi wa TACTIC.
"Baadhi ya barabara wakati wa mvua zimekuwa hazipitiki, mitaro imekuwa inafurika maji na kusababisha mafuriko, napenda kutoa shukrani zangu kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuiona changamoto hii na kuleta mradi huu utakaosaidia kuboresha shughuli za usafiri na usafishaji", alisema.
Aliongeza kuwa kupitia stendi hiyo ya kisasa uchumi utaimarika na ajira zitaongezeka kwani kutakuwa na vibanda vya kukatia tiketi, biashara, mama lishe na pia mapato yataongezeka kutoka shilingi milioni 40 kwa mwaka ambapo wanatarajia baada ya stendi kukamilika watakusanya zaidi ya shilingi milioni 250 kwa mwaka.
Naye, Mratibu wa mradi wa TACTIC Mhandisi Charles Ibengwe alisema kuwa fedha za mradi huo ni mkopo nafuu toka Benki ya Dunia huku mradi ukihusisha ujenzi wa stendi ya mabasi, ujenzi wa barabara ni Km 4.89, mifereji ya maji ya mvua Km 8.15 pamoja na ujenzi wa jengo la ofisi ya usimamizi wa mradi ambapo wanatarajia mradi utakamilika mwezi Oktoba 2026.
Kwa upande wake, Meneja wa TARURA wilaya ya Babati Mhandisi Aloyce Nombo alieleza kuwa kukamilika kwa barabara hizo kutaongeza mtandao wa barabara za lami hadi kufikia Km 18.9, ukilinganisha na Km 14.2 zilizokuwepo. Pia kutakuwa na ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua katika kata ya Maisaka, Singe na Bagara itakayosaidia kuondoa adha ya maji yanayopita katika makazi ya watu na pia taa zikiwekwa wananchi watafanya kazi hadi usiku na taa hizo zitaimarisha usalama.
Naye, mkazi wa mtaa wa Gendikuu Bi. Sara Nzowa ameishukuru serikali kwa ujenzi wa mifereji kwani awali kipindi cha mvua maji yalikuwa yanaleta athari yanaingia ndani kwenye makazi ya watu, mifugo ilikufa ilienda na maji na mashamba yaliathirika lakini sasa ujenzi wa mifereji utasaidia kuondoa adha hiyo.
Vilevile, Bw. Issa Seif mkazi wa mtaa wa Babati ameishukuru serikali kwa matengenezo ya barabara za lami Babati mjini pindi zitakapokamilika barabara hizo zitasaidia kupendezesha mji na watafanya biashara bila wasiwasi huku taa zikiwekwa watafanya kazi hadi usiku na usalama utaongezeka.
Aidha, Bw. Abdulrahman Issa mkazi wa mtaa wa Sawe alisema kuwa tangu watangaziwe kutakuwa na ujenzi wa barabara ya lami katika eneo lao thamani ya ardhi imepanda na wapangaji wanaongezeka pia mradi ukikamilika uchumi wa wananchi wa maeneo hayo utaongezeka kwani barabara hiyo ni njia ya kuelekea barabara kuu ya Arusha.
Naye, Bw. Justin Majagi mkazi wa Babati ambaye amepata kazi katika ujenzi wa stendi ya mabasi ameishukuru serikali kwa mradi huo uliowasaidia vijana kama yeye kupata ajira inayomsaidia kuendesha maisha na kupata kipato.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...