MWANASHERIA Mkuu wa Serikali Hamza Johari amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kamati ya Taasisi ya Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) , Balozi Wilson Masilingi, tarehe 14 Aprili, 2026 katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bungeni, Jijini Dodoma.

Balozi Masilingi ambaye aliteuliwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI Januari 29, 2026 amemtembelea Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kujitambulisha na kumpongeza kwa kutekeleza kwa ufanisi majukumu ya kuishauri Serikali katika masuala ya kisheria Nchini.

Aidha, katika Kikao hicho, Viongozi hao wamejadiliana namna bora ya kuimarisha zaidi Ushirikiano uliopo baina ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na TEITI.

Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya TEITI aliambatana na Katibu Mtendaji wa TEITI Mariam Mgaya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...