MOSHI.
MWILI wa mtoto wa miezi mitatu Dorin Edward uliokuwa umezikwa kimakosa katika kitongoji cha Madi kusini kijiji cha Korini kusini Kata ya Mbokomu wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro umefukuliwa na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Mieresini mji mdogo wa Himo.
Tukio hilo limejiri leo baada ya chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya Rufaa ya mkoani wa Kilimanjaro Mawenzi kujichanganya na kukabidhi wafiwa mtoto ambao sio wao.
Akizungumza mama mzazi wa Dorin, Neema Gwatu alisema kuwa, mwanae huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua (Nimonia) ambapo walimpeleka katika kituo cha Afya cha Himo (OPD).
Neema aliendelea kudai kuwa, mnamo Aprili 9 mwaka huu majira ya saa nne usiku mtoto alihamishiwa katika hospitali ya Mawenzi kwa matibabu zaidi na Aprili 10 majira ya saa tano asubuhi mtoto alifariki.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...